ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, August 20, 2013

NI EAST BOYZ MWBINGWA U15 NAO ALLIANCE ACADEMY MABINGWA WA U17 KOMBE LA ALLIANCE AFRICA

Mwenyekiti wa Chama Cha Soka Mkoa wa Mwanza (MZFA) Jackson Songora akimkabidhi kombe la Ubingwa wa U17 mchezaji wa Alliance Academy Hadji Vemba mara baada ya timu hiyo kuibamiza timu ya Spares kutoka Kenya  mabao 5-0 kwenye mchezo wa fainali Alliance Africa uliofanyika katika uwanja wa Nyamagana jijini Mwanza.
NA ALBERT G. SENGO: MWANZA
Mashindano ya soka kwa timu za Alliance Africa yaliyoanza kutimua vumbi mwishoni mwa wiki iliyopita kwenye Uwanja wa Nyamagana jijini Mwanza leo yamefikia tamati kwa East Boyz ya Mwanza Tanzania kunyakua ubingwa wa U15 mara baada ya kuifunga Alliance Academy nayo ya jijini Mwanza bao 4-3, katika mchezo uliolazimu kuingia katika hatua za matuta. 

Haikuishia hapo mchezo uliokuwa ukisubiriwa kwa hamu ni ule wa U17 baina ya timu mbili kutoka nchi mbili tofauti, wenyeji Alliance Academy ya Mwanza Tanzania na timu ya Spares kutoka nchini Kenya mchezo ulioishia kwa wenyeji Alliance Academy kutawazwa mabingwa kwa kuifurumusha Spares bao 5-0 (SIKILIZA TAARIFA ZAIDI KWA KUBOFYA BOFYA PLAY)


Heka heka langoni mwa Spares iliyozaa goli la 3.

Kocha wa Alliance Academy Ahmed Simba akitoa maelezo kwa wachezaji wake nini cha kufanya kabla ya kuingia kipindi cha pili ambapo timu hiyo iliibuka na ushindi mnono wa mabao 5-0 dhidi ya Spares toka Kenya na kunyakua ubingwa wa Alliance Africa Under 17.

Kocha wa Spares ya Kenya Shem Kado akitoa maelezo kwa wachezaji wake nini cha kufanya kabla ya kuingia ungwe ya pili, hata hivyo timu hiyo ilishindwa vibaya na kuambulia kichapo cha mabao 5-0 toka kwa mabingwa Alliance Academy Mwanza.

Alliance Academy Mwanza wakishangilia moja ya magoli yao kwenye mchezo huo wa fainali.








Picha ya pamoja Alliance na Spares .

Sherehe tupu ....


Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.