ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, July 12, 2013

CROWN PAINTS YAFUNGUWA TAWI JIPYA MWANZA

Mkurugenzi wa Crown Paints Ramesh Rao akizungumza na waandishi wa habari juu ya ujio wa kampuni yake nchini Tanzania.
Kampuni ya utengenezaji na uuzaji wa rangi aina ya Crown Paints toka nchini Kenya leo imefunguwa tawi lake jipya mkoani Mwanza ili kupanua soko lake nchini Tanzania na kuleta ustawi wa wananchi wa Afrika Mashariki.

Ujio wa Crown Paints nchini Tanzania umekuja kukidhi mahitaji ya uboreshaji wa kudumu wa muonekano wa majengo ndani na nje hasa ukizingatia miji na majiji mengi nchini yameshuhudia kasi ya ujenzi wa majengo mapya sambamba na nyumba nyingi mpya za kisasa hivyo Crown Paint imekuja wakati muafaka kuuza bidhaa bora zenye kulinda na kuleta uthamani halisi wa majengo hayo.
Afisa Uhusiano wa Crown Paints Bi. Elly Fred akitoa ufafanuzi mbele ya waandishi wa habari waliohudhuria uzinduzi katika Ukumbi wa JB Belmont jijini Mwanza.
Kampuni ya Crown Paint ilianzishwa mnamo mwaka 1958 Nairobi nchini Kenya nakuendelea kutanua soko lake kwa nchi mbalimbali Afrika Mashariki na nchi za COMESA.

Ilifungua tawi lake la kwanza nchini Tanzania mkoani Arusha mwezi july mwaka jana (2012) huku ikisambaza bidhaa zake katika mikoa mbalimbali ikiwemo Mwanza.

Hivyo ujio huu utatoa fursa  kwa wakazi wa Mwanza na Kanda ya Ziwa kupata bidhaa kwa bei nafuu zaidi na kujichagulia aina za rangi wanazotaka kulingana na mahitaji.
Afisa Uhusiano na Masoko wa Crown Paints Bi. Elly Fred akitoa ufafanuzi mbele ya waandishi wa habari waliohudhuria uzinduzi katika Ukumbi wa JB Belmont jijini Mwanza.
"Tuna rangi za kupamba nyumba ndani na nje, tuna rangi za magari na vilevile tuna rangi kwaajili ya vyuma, bidhaa nyingi zikitengenezwa toka kiwanda chetu kilichopo nchini Kenya na nyingine tukiziagiza toka Afrika ya Kusini na Uingereza ambapo zinauzwa kupitia jina na nembo yetu nasi tukitumika kuzisambaza sokoni"  alisema Bi Elly.
Bw. Stanley Kipkoech ambaye ni Meneja Masoko wa Crown Paints akizungumza na wandishi wa habari waliohudhuria uzinduzi huo. 
"Tuna mpango na tayari tumewaelekeza watafiti wetu kutembelea maeneo mbalimbali ya huduma za kijamii kama Shule, Vituo vya afya na kadhalika ili kubaini changamoto mbalimbali zinazokabili maeneo hayo na ndani ya miezi michache ijayo tutakuwa na kampeni ya kuboresha shule angalau 4 na vituo viwili vya afya vilivyopo ndani ya mkoa wa Mwanza" alisema Bw. Stanley.
Biidhaa za Crown Paints
The goal is to capture at least 50 per cent of the Tanzania paint market. This will partly entail setting up depots and mini plants to serve the rising demand for paint as the Tanzanian government and private sector invest more in infrastructure.

"We will leverage or superior brand quality supported by strong reseach and development to successfully rollout in the Tanzanian market," added Rao.
Wanahabari.

Tupe maoni yako

1 comments:

Note: Only a member of this blog may post a comment.