Mkuu wa mkoa wa Mwanza Evarist Ndikilo akipiga penati ndogo kuashiria uzinduzi wa hafla ya ukabidhi vifaa kwaajili ya michuano ya Pepsi Meya's Cup 2013, huku Mstahiki Meya wa jiji la Mwanza Stanslaus Mabula akishuhudia tukio hilo lililofanyika katika uwanja wa Nyamagana.
Injinia Evarist Ndikilo.
NA ALBERT G. SENGO: MWANZA
Timu 19 zitakazoshiriki Meya's Cup2013 tayari zimekwisha kabidhiwa vifaa vya michezo kuweza kushiriki michuano hiyo kwa mwaka huu.
Akikabidhi vifaa hivyo kwa makapteni wa timu zote shiriki pamoja na waamuziwa michuano hiyo inayotaraji kuanza kutimua vumbi mnamo tarehe 15 mwezi huu (juni) 2013, Mkuu wa mkoa wa Mwanza Evarist Ndikilo amesisitiza nidhamu mchezoni na kuwataka vijana washiriki kujibidiisha kuusaka ushindi ili wajinyakulie zawadi ambazo zimenuia kusaidia kuboresha mitaji yao sambamba na kuwaandaa kuifanya michezo kuwa sehemu ya ujasiliamali.
Kila timu imekabidhiwa jezi seti moja ikiwa na soksi zake pamoja na mpira mmoja kwa kila timu nazo zawadi kwa washindi zikianikwa nao wadau kujionea.
Mgeni rasmi wa siku ya Uzinduzi ni Katibu Mkuu wa TFF Angetile Osiah.
Katika hatua nyingine kwa kutambua mchango wa maendeleeo ya michezo nchini Kampuni ya My Way Entertainment ambao ni waandaaji wa Meya's Cup 2013wamemwalika Mwanamichezo wa Sports Xtra Mbwiga wa Mbwiguke.... Zaidi bofya msikilize.
Miss Nyamagana Rosemary Peter (kushoto) akimwongoza mrembo mwenzake kuonyesha baadhi ya vikombe vya washindi michuano ya Meya's Cup 2013, hapa Rose alikuwa na kombe litakalotwaliwa na timu yenye nidhamu na mwenzie akionyesha kiatu cha dhahabu kitakachotwaliwa na mfungaji bora.
Viongozi pamoja na wadau wa soka Mwanza.
Safu ya mbele ni waandaaji wa Michuano hii My Way Entertainment na nyuma yake ni warembo washiriki wa Miss Mwanza watakaochuana mnamo Ijumaa ya wiki hii tarehe 14 Juni ndani ya Yatch Club Mwanza.
Ni kombe, vikombe pamoja na medali zikichagizwa na tabasamu warembo washiriki wa Miss Mwanza watakaochuana mnamo Ijumaa ya wiki hii tarehe 14 Juni ndani ya Yatch Club Mwanza ile hali mbele kabisa timu waandaaji My Way Entertainment ikiwa tayari kutoa mwongozo.
Kila timu ilikabidhiwa mpira mmoja kwaajili ya mazoezi.
Safu ya wadau wa michezo Mwanza ikiwa imeketi jukwaani.
Seti za jezi kwa kila timu.
Makombe na medali za washindi.
Sports warembo wakiwa na zawadi za mipira iliyokabidhiwa kupitia maswali kwa wadau wa soka waliohudhuria makabidhiano hayo yaliyofanyika uwanja wa Nyamagana jijini Mwanza, kulia kabisa ni Miss Mwanza 2012 anayetaraji kuliachia taji lake ijumaa hii (14 juni) Yatch Club.
REA KUSAMBAZA MITUNGI YA GESI 19,530 MKOANI SINGIDA
-
-Wananchi 3,255 kila wilaya ya mkoa huo kunufaika
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kupitia Wakala wa Nishati
Vijijini (REA); kuanzia tarehe 20 ...
MALIZA WIKENDI YAKO NA MERIDIANBET
-
KAMA unataka kumaliza wikendi yako vizuri leo hii, wewe suka jamvi lako na
wakali wa ubashiri Meridianbet ambapo nafasi ya kuibuka bingwa unayo leo
maa...
Arusha Yasimama Kwenye Maombi: Miaka 63 ya Uhuru
-
Viongozi wa dini ,mkuu wa mkoa wa Arusha Paul Makonda na wananchi
wakiendelea na maombi katika matembezi ya kuombea mkoa wa Arusha na
maathimisho ya mi...
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.