Wadau wa habari vituo vya televisheni nchini. |
TAARIFA KWA
VYOMBO VYA HABARI
Chama
Cha Waandishi wa Habari mkoa wa Mwanza kimeandaa harambee ya kuchangisha
shilingi milioni mia moja
(100,000,000/-) kwa ajili ya kununua mtambo wa kuchapa magazeti ili
kukiwezesha chama kuwa na mradi wake ambao utasaidia kukiingizia chama kipato.
Pamoja
na kuingiza kipato cha chama mradi huo utakiwezesha chama kuanzisha gazeti la
kijamii ambalo litakuwa na jukumu la kuandika habari za kijamii na za vijijini
zaidi kwa ajili ya mikoa ya kanda ya ziwa zitakazosaidia kuchochea maendeleo ya
jamii.
Chama
kina wajibu wa kuhakikisha kuwa jamii ya wananchi wa Mkoa wa Mwanza na kanda ya
ziwa wanapata haki yao ya kupata habari sahihi kwa wakati na zinazohusu
shughulli za maendeleo yao ambazo ni chachu muhimu kwa maendeleo ya jamii yeyote
ile.
Katika
kutekeleza jukumu la kuwapatia mazingira mazuri ya kuwafikishia wananchi habari
sahihi na kwa wakati chama kimekuwa kikikabiliwa na changamoto ya upatikanaji
na uchapishaji wa habari za vijijini na zile zinahusu shughuli za kijamii,
ambazo ni muhimu kwa maendeleo ya jamii yetu na taifa kwa ujumla.
Ili
kukabiliana na changamoto hiyo Chama cha Waandishi wa habari Mkoani Mwanza
kimeandaa harambee kwa ajili ya kupata shilingi milioni mia moja
(100,000,000/-) kwa ajili ya kununua Mtambo wa kcuhapa magazeti. Mtambo huu
utakiwezesha chama kufufua gazeti lake la TAA pamoja na kufanya kazi zingine za
nje kama chanzo cha mapato kwa chama.
Harambee
hiyo itafanyika tarehe 04/05/2013 katika Ukumbi wa JB BELMONT Hotel ambapo
wadau mbali mbali wa habari wakiwemo wafanyabiashara, viongozi wa vyama na
serikali, wakuu wa mashirika na taasisi mbali mbali za umma na binafsi ili
kufanikisha harambee hiyo.
Tumewaalika
wananchi wa kada mbali mbali wa Mkoa wa Mwanza kushiriki katika Harambee hii
kwa sababu kama MPC tunaamini kwamba Chama kiko kwa ajili ya wananchi ili
kuwatumikia wananchi wa mkoa wa Mwanza na kanda ya Ziwa. Ushiriki wao ni ishara
ya umiliki wao wa mchakato huu na sisi kama chama ni waratibu na wasimamizi tu
wa shughuli hii lakini katika hali halisi waandishi wote wa wana Mwanza ndio wamiliki halisi wa mtambo utakaonunuliwa
na hata gazeti litakaloanzishwa.
Mgeni
rasmi ambaye ataongoza harambee hiyo atakuwa ni Ridhiwan Kikwete.
Mwanza
Press Club (MPC) ni chama cha Waandishi wa habari Mkoani Mwanza ni taasisi
isiyo ya kiserikali inayowaleta pamoja waandishi wa Mkoa wa Mwanza katika
kutekeleza majukumu yao kwa weledi na kuzingatia maadili ya taaluma hiyo.
Deus Bugaywa
Mwenyekiti
Mwanza Press Club
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.