ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Sunday, April 7, 2013

PPF YAKABIDHI VIFAA KUMALIZIA UJENZI KITUO CHA POLISI NYAKOTO MKOANI MWANZA

Meneja wa PPF Kanda ya ziwa Meshack Bandawe akimkabidhi mifuko ya simenti Kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza Ernest Mangu, mchango wenye thamani zaidi ya shilingi milioni 2, kwaajili ya kuchangia uharakishwaji wa ujenzi wa kituo cha polisi Nyakato jijini Mwanza. 


Mwenyekiti wa kamati ya ujenzi wa kituo cha polisi Nyakato Bw. Alfred Wambura, amesema kuwa kamati yake imenuia kuhakikisha ujenzi wa kituo hicho unakamilika mwishoni mwa mwezi wa 5 na kukabidhiwa kwa jeshi la polisi.

Mikakati mingine iliyowekwa na kamati hiyo ni kukamilisha ujenzi wa nyumba ya makazi ya OSS wa Nyakato pamoja na watendaji wengine watatu wanaomfuata kwa cheo, ili kurahisisha utendaji wa kila siku wa shughuli za usalama wa jeshi hilo. 


Meneja wa PPF Kanda ya ziwa Mesharck Bandawe amesema kuwa ulinzi kwa maisha ya baadaye ya mwananchi uko ndani ya  mfuko wa uwekezaji wa PPF,  na ulinzi wa wananchi na mali zao uko chini ya jeshi la polisi hivyo amewataka wadau wengine wa mashirika mbalimbali kujitokeza kulisaidia jeshi hilo kukamilisha shughuli za utendaji kwa manufaa ya ustawi wa jamii.


Wadau wa PPF wakisikiliza kwa makini yanayojiri kwenye makabidhiano hayo.


Diwani wa kata ya Mahina, Mhe. Chinchibela ametoa rai kwa mashirika mengine kusaidia jeshi la polisi kama sehemu ya ulinzi shirikishi, kwani msaada huu wa PPF umekuwa wa tatu kutoka kwa mashirika mbalimbali mkoani Mwanza ambayo yamethubutu kukisaidia kituo hicho. 


Mhe. Manyerere ambaye ni diwani wa kata ya Nyakato ameishukuru asasi ya PPF kusaidia kuchangia ujenzi wa kituo cha polisi Nyakato ambacho ni moja kati ya vituo muhimu kwani kinahudumia usalama wa maeneo ya kata takribani 4 za jiji la Mwanza. 


Mifuko ya simenti iliyotolewa na PPF ikishushwa kutoka kwenye roli. 


Meneja wa PPF Kanda ya ziwa Meshack Bandawe akiteta jambo na Kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza Ernest Mangu mara baada ya makabidhiano kukamilika.


Kamanda akifanya ukaguzi kwa shughuli za ujenzi zinazoendelea kituoni hapo. 


Hiki ni chumba cha mahabusu ambacho kwa mujibu wa kamati ya ujenzi kitakuwa na choo kukidhi usumbufu na changamoto zilizojitokeza katika vituo vingine.


Ukaguzi ukiendelea...


Maelekezo toka kamati ya ujenzi.


Ujenzi ukiendelea na mchango wa PPF kama unavyoonekana.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.