ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, April 25, 2013

KALA JEREMIAH, H. BABA, KITALE, HARDMAD, KABAGO, DARK MASTER, MZIWANDA, DAYNA NA MWANZA KWANZA WASHIRIKI ZOEZI LA KUSAFISHA MAZINGIRA MAKABURI YA MV. BUKOBA

Baadhi ya wasanii wa nyanja za Muziki wa Bongo Fleva, filamu na maigizo walipoungana leo jijini Mwanza kusafisha mazingira ya makaburi ya watu waliofariki kupitia ajali ya Mv. Bukoba mara baada ya kukuta mazingira ya eneo hilo hayaridhishi.

Hivi ndivyo hali ilivyokuwa kwa eneo la makaburi haya ya kumbukumbu ya makaburi ya baadhi ya waliofariki dunia kwenye ajali ya meli ya Mv. Bukoba iliyozama kwenye ziwa Victoria Mei 21 1996.

Shughuli zilianzia hapa eneo makaburi ya mwanzo

H. Baba akiwa akipalilia kuondoa nyasi kwenye moja ya makaburi ya waliofariki Mv. Bukoba huku akipata ushirikiano toka kwa wadau wengine toka Mwanza Kwanza kama vile Producer Shaib (mwenye miwani).

Hatua kwa hatua shughuli iliendelea kuonekana.

Wadau wengine hususani wamaeneo ya karibu na makaburi walidiriki kuja na watoto wao kushiriki zoezi la usafi kama mtoto huyu anavyoonekana pichani (jina litapatikana tu).

Kijana huyu naye alikuwa sehemu ya jumuiko la usafi hapa makaburini, nyuma wakionekana Hardmad, Producer wa One love Production na Mwan Mwanza Kwanza.

Msanii wa sanaa ya maigizo nchini Kitale ambaye vilevile ni msanii wa Bongo fleva alishiriki vyema kufanya usafi kwenye eneo la makaburi ya watu waliofariki dunia kwenye ajali ya meli ya Mv. Bukoba iliyozama kwenye ziwa Victoria Mei 21 1996.

Hardmad alikuwa akichagiza huku akiimba ili kujipa ujasiri kwani zoezi lilipoonekana kuwa gumu ilibidi kila mmoja eneo la tukio kugawiwa makaburi matatu matatu kuharakisha zoezi la usafi kwenye eneo la makaburi ya watu waliofariki dunia kwenye ajali ya meli ya Mv. Bukoba iliyozama kwenye ziwa Victoria Mei 21 1996.

Producer wa One Love Production akihusika na usafi nyuma yake ni Kala Jeremiah naye akiwajibika kwani zoezi lilipoonekana kuwa gumu ilibidi kila mmoja eneo la tukio kugawiwa makaburi matatu matatu kuharakisha zoezi la usafi kwenye eneo la makaburi ya watu waliofariki dunia kwenye ajali ya meli ya Mv. Bukoba iliyozama kwenye ziwa Victoria Mei 21 1996.

Wana Mwanza Kwanza nao waliibuka kusaidia zoezi.


Kutoka kulia ni Mc. Mziwanda, H. Baba, Kala Jeremiah, Philbert Kabago na Kitale.

Shughuli ikiendelea.

Kutoka kushoto ni H. Baba, Dark Master na msanii toka Mwanza Kwanza.

Zoezi la usafi  likiendelea kwenye eneo la makaburi ya watu waliofariki dunia kwenye ajali ya meli ya Mv. Bukoba iliyozama kwenye ziwa Victoria Mei 21 1996.

  Sala maalum ilihusishwa kuwakumbuka watu waliofariki dunia kwenye ajali ya meli ya Mv. Bukoba iliyozama kwenye ziwa Victoria Mei 21 1996.

Kitale akiswali salaa maalum.

Katika sala watoto na Kitale.

Lango kuu na utambulisho wa eneo la makaburi ya baadhi ya waliokufa maji kwenye ajali ya meli ya Mv. Bukoba iliyozama kwenye ziwa Victoria Tarehe 21 Mei 1996.

Kala Jeremia ni mmoja kati ya wasanii wa Mwanza walioongoza zoezi hilo kufanyika kwa ufanisi, Ijumaa Hii anategemea kufanya uzinduzi wa Album yake ijulikanayo kwa jina 'Pasaka' ndani ya Villa Park. 
NA ALBERT G. SENGO: MWANZA

Wasanii wa muziki wa Nyumbani (Bongo Fleva) Kala Jeremiah, H. Baba, Kitale, Hardmad, Philbert Kabago, Dark Master na mwanadada Dayna leo wameshiriki zoezi la kusafisha mazingira ya makaburi ya watu waliofariki dunia kwenye ajali ya kuzama kwa meli ya Mv. Bukoba, makaburi yaliyoko Igoma nje kidogo ya jiji la Mwanza.

Zoezi hilo limekuja mara baada ya mmoja kati ya wasanii hao (H. Baba) kupita katika eneo hilo na kujionea hali mbaya ya mazingira ndipo alipochukuwa jukumu la kuwasilisha taarifa hiyo kwa wasanii wenzake ambapo uungwaji mkono ulikuwa wa asilimia mia moja.

Mapema leo shughuli za usafi zilianza kushika kasi, zoezi ambalo liliwachukuwa takribani masaa manne kumalizika likuwa gumu kutokana na magugu na nyasi nyingi kumea kwenye eneo hilo la makaburi kiasi cha kuwasababisha wasanii hao kuongeza zana zaidi za usafi ili kuweza kufikia lengo lao.


Tupe maoni yako

1 comments:

  1. MMEONYESHA MFANO MZURI, HIVI JUKUMU LAKUTUNZA HAYA MAKABURI LIKO CHINI YA NANI?

    ReplyDelete

Note: Only a member of this blog may post a comment.