ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, March 4, 2013

LEO DUNIA YAADHIMISHA KUZALIWA KWA MAMA AFRIKA


Miriam Makeba (4 March 1932 – 9 November 2008), almaarufu kama Mama Africa, huyu ni mtunukiwa wa tuzo za Grammy- akishinda kama mwimbaji na mwanaharakati wa haki za kiraia Kusini mwa Afrika.
Kwenye miaka ya 1960s alikuwa ni mwanamuziki wa kwanza toka Afrika muziki wake kupenya na kutawala himaya ya muziki nchini Marekani na dunia kwa ujumla.  "Pata Pata", ndiyo wimbo wimbo uliomtambulisha aliurekodi mwaka 1957 na kuuachilia rasmi nchini marekani mwaka 1967. Aliurekodi wimbo huo na kualikwa kwenye matamasha mengi akiambatana na waimbaji maarufu wa enzi hizo kama vile Harry BelafontePaul Simon, na jamaa ambaye aliwahi kuwa mumewe wa kwanza Hugh Masekela.
Alishiriki kikamilifu kampeni dhidi ya mfumo wa ubaguzi wa rangi nchini Afrika Kusini. Matokeo yake serikali ya nchi hiyo ilibadili maamuzi na kumnyang'anya uraia wake na haki ya kurudi nchini humo, tukio lililotokea mwaka 1959. Badaye 1990, Kamba za mfumo wa kibaguzi zilipokatika ndipo kwa mara ya kwanza tena akarudi nyumbani.
Miriam Makeba alikutwa na mauti baada ya kupata shinikizo la damu mnamo tarehe 9 November 2008 ikiwa ni mara baada ya kumaliza kutumbuiza kwenye tamasha lililoandaliwa nchini Italia kuungamkono kampeni ya mwandishi wa vitabu Roberto Saviano aliyekuwa na msimamo wake wa kupinga genge la mafia la Camorra, lililoshiriki kuwauwa wahamiaji toka nchini Ghana.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.