ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, March 18, 2013

KAMATI YA MAUDHUI TCRA YAKUTANA NA BAADHI YA WAANDISHI WA HABARI MWANZA.

Makamu mwenyekiti wa Bodi ya Kamati ya Maudhui toka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania Mzee. walter Bugoya akiongoza mkutano wa ziara ya kamati hiyo uliofanyika leo ukumbi wa Hotel Gold Crest mkoani Mwanza, pichani wengine kuanzia kulia ni Bi. Eunice Mabagala, Eng. Lawi Odiero ambaye ni meneja wa kanda, Bw. Abdul Ngalawa (mjumbe), na mwisho kabisa ni Joseph Mapunda (Mjumbe).


Mjumbe wa Kamati ya Maudhui ya Mamlaka ya mawasiliano Tanzania Abdul Ngalawa akitoa mchango wake katika mkutano kamati ya Maudhui ya TCRA na waandishi wa habari wa baadhi ya vyombo mkoani Mwanza, uliofanyika leo ukumbi wa Hotel Gold Crest , Kamati hiyo imeundwa kwa mujibu wa sehemu ya 4 ibara ya 26 (1) ya sheria namba 12 ya Mamlaka ya Mawasiliano ya mwaka 2003.

Kwa mujibu wa sheria kazi za Kamati ya Maudhui ni pamoja na Kumshauri waziri wa sekta kuhusiana na sera ya utangazaji nchini, Kushughulikia malalamiko kutoka kwa watangazaji na watumiaji wa huduma za utangazaji nchini na Kusimamia na kuhakikisha kuwa kanuni za utangazaji zinafuatwa.

Waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali Mwanza wakifuatilia shughuli za mkutano huo leo.

Eng. Lawi Odiero ambaye ni meneja wa kanda akijibu moja kati ya hoja zilizowasilishwa na waandishi wa habari kama sehemu ya maswali kwenye mkutano baina ya Kamati ya Maudhui ya TCRA na Waandishi wa habari wa baadhi ya vyombo mkoani Mwanza, uliofanyika leo ukumbi wa Hotel Gold Crest

Wanahabari kusanyikoni.

Bi. Eunice Mabagala akitoa ufafanuzi.
Moja ya kazi ya Kamati ya Maudhui ni kumshauri Waziri wa Sekta kuhusiana na sera ya utangazaji nchini.Ili kutekeleza azma hiyo Kamati inafanya ziara katika mikoa mbalimbali nchini kukutana na watangazaji na watumiaji wa huduma zautangazaji ili waweze kubadilishana mawazo ya jinsi ya kuboresha sekta ya utangazaji nchini.

Maeneo ambayo Kamati itayaangalia ni pamoja na:-
1.Matumizi ya vyombo vya habari katika kuchochea uvunjifu wa amani na kuweka hali ya utengamano,

2.Matumizi sanifu ya Lugha ya Kiswahili,

3.Kubadilisha maudhui ya vipindi vinavyotangazwa na vyombo kutoka katika maudhui ya mapenzi na burudani kwenda katika maudhui ya kupenda kufanya kazi  na kuwajengea moyo wa kujiaminikatika kujiletea maendeleo,

4. Kuwafahamisha watumiaji wa huduma za utangazaji kuwa wanayohaki ya kulalamikia maudhui ambayo si sahihi au yanayokiuka maadili ya utangazaji. Malalamiko hayo yanatakiwa yapelekwe katika ofisi za Mamlaka ya MawasilianoTanzania ili yafanyiwe kazi.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.