Kwa mujibu wa meneja wa Bia ya safari Oscar Shelukindo amesema kuwa lengo la mashindano hayo ambayo yanatimiza miaka 6 sasa tangu kuanzishwa kwake ni kuboresha Afya za walaji ambao ni wananchi kwa kuzingatia ubora na kanuni za afya.
Vilevile Shindano hilo la nyama choma limenuia kuongeza uelewa kwa waandaaji wa nyama choma nchini.
Shindano hilo la nyama choma linatoa uelewa kuanzia vifaa bora vya kutumia wakati wa kuandaa nyama choma, moto utakaotumika, waya malum wa kuchomea nyama, usafi wa mchomaji mwenyewe na uchangamfu wake kwenye biashara.
"Mwezi uliopita mwishoni nilikuja kuendesha semina elekezi ambayo tuliongelea vigezo na taratibu zote ambazo zinahusiana na uchomaji wa nyama kwa washiriki wa shindano pamoja na wengine wa baa mbalimbali ambao walijitokeza kwa wingi ili kupata nafasi kujifunza mbinu mbalimbali na kanuni zake kuboresha suala zima la uchomaji nyama hivyo ni yangu matumaini si siku nyingi mtaona mabadiliko ya ubora kwa bar nyingi za hapa jijini Mwanza" alisema Sakibu ambaye ni jaji wa shindano hilo.
Meneja mauzo wa bia ya Safari Lager Kanda ya Ziwa Malaki Sitaki akizitaja zawadi. |
Mshindi wa Kwanza atajipatia kitita cha shilingi milioni 1,
Mshindi wa pili shilinhi laki 8,
Mshindi wa tatu shilingi laki 6,
Mshindi wa nne shilingi laki 4, na
Mshindi wa tano shilingi laki 2.
Wakazi wa Mwanza na vitongoji vyake wameombwa kujitokeza kwa wingi kushuhudia ni baa ipi itanyakuwa ushindi katika Safari Lager Nyama Choma Competition mkoa wa Mwanza huku wakipata ladha safi ya bia ya Safari iliyonyakuwa hivi karibuni tuzo za Bia bora Afrika katika mashindano yaliyofanyika Acra nchini Ghana.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.