|
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Evarist Ndikilo akizungumza kwenye kikao maalum. |
SERIKALI Mkoani Mwanza
imetekeleza Agizo la Waziri Mkuu Mizengo Pinda alilolitowa wakati wa
kusuluhisha mgogoro wa kiimani wa uchinjaji kitoweo kwa kusimamia uundwaji wa
Kamati ya Pamoja ya madhehebu ya Kikristo na Kiislamu ili kushughulikia mgogoro
wa kidini wa uchinjaji ulioibuka hivi karibuni katika maeneo ya Kanda ya Ziwa.
Kamati hiyo ya pamoja
iliyoundwa na wajumbe ishirini kutoka madhehebu makuu mawili ya Kikristo na
Kislamu Mkoani humo ambapo Waziri Mkuu Pinda alitoa ushauri kwa serikali ya
Mkoa kupita Kamati yake ya ulinzi na usalama Februari 16 mwaka huu kuunda
kamati maalumu baada ya kutokea vurugu na mauaji huko katika Mji wa Buseresere
Mkoani Geita.
|
Wawakilishi upande wa Waislamu mkoa wa Mwanza. |
|
Wawakilishi wa upande wa Wakristo |
|
Sehemu waliyoketi viongozi mbalimbali na waandishi wa Habari. |
Akizungumza na vyombo vya habari katika ukumbi wa ofisi yake, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Injinia Evarsti Ndikilo alieleza kwamba Kamati hiyo ya pamoja iliyoundwa na ukuzinduliwa jana ya madhehebu hayo mawili yenye wajumbe ambapo kila upande utawakirishwa na wajumbe wasiozidi kumi ambayo imekutana na kushauriana na Kamati ya ulinzi na usalama Mkoa wa Mwanza.
|
Mwenyekiti wa Kamati Sheikh Hassan Kabeke. |
Baada ya kuzinduliwa
Kamati hiyo iliwachagua viongozi wake ambao pia wataunda Kamati ndogo ya watu wanne
ambapo itatoa wajumbe wawili kila upande, Mwenyekiti wa Kamati hiyo amechaguliwa
kuwa Sheikh Hassan Kabeke, Mwakamu wake ni Askofu Charles Sekelo, Katibu Askofu
Zenobius Isaya na Msaidizi wake ni
Sheikh Mohamed Bara.
|
Katibu wa Kamati Askofu Zenobius Isaya akizungumza na vyombo vya habari mara baada ya kikao kumalizika. |
Baada ya kuzinduliwa Kikao hicho kilitoa maazimio matano ikiwa ni pamoja na kuundwa kwa Kamati ndogo ya viongozi
wanne ambao kazi yao ni kuratibu na
kuangalia mambo muhimu yatakayo shughulikiwa na kujadiliwa kabla ya kufikishwa
kwenye Kamati ya wajumbe ambayo itayajadili kwa umakini kisha kupeleka
mapendekezo yake kwa Kamati ya Serikali kujadiliwa kwa pamoja na kutolewa
maamuzi.
|
Ishara ya maafikiano. |
|
Mkuu wa mkoa wa Mwanza Everist Ndikilo hapa salimiana kwa ukaribu zaidi na baadhi ya viongozi wawakilishi walioshiriki kikao hicho. |
|
'Hii ndiyo jadi ya amani ya watanzania tuliyoizoea' kutoka kushoto ni Katibu wa Baraza la Waislamu (BAKWATA) mkoa wa Mwanza Shekhe Mohamed Salum Mbala, Katibu wa Kamati iliyoundwa Askofu Zenobius Isaya akiwa na Mwenyekiti wake Sheikh Hassan Kabeke wakifurahi kwa pamoja ndani ya mazungumzo yao. |
|
Ni mwendo wa kubadilishana mawasiliano. |
|
Ni kama vile anasema "Kwa hili tendeka leo hata Mwenyezi Mungu anafurahi pamoja na malaika wake huko juu" |
|
Picha ya pamoja ya Wakuu mbalimbali na Kamati iliyoundwa . |
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.