Bw. Habbi Gunze |
Zimesalia siku 3 tu
ambapo Mamlaka ya Mawasiliano nchini TCRA itachukuwa hatua ya kuzima mitambo ya
utangazaji wa televisheni ya mfumo wa analojia kwa mkoa wa Mwanza.
Hayo yamebainishwa leo
jijini Mwanza na Mkurugenzi wa Utangazaji wa Mamlaka ya Mawasiliano nchini Bw.
Habbi Gunze wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini humo kuhusiana na
utekelezaji wa hatua hiyo kwa mujibu wa makubaliano ya nchi wanachama wa
jumuiya ya Afrika Mashariki ambapo amesema kuwa ifikapo tarehe 28 februari 2013
zoezi hilo litafanyika kwa mkoa wa Mwanza.
Msikilize Mkurugenzi wa Utangazaji TCRA akibainisha maeneo yatakayoguswa na zoezi hilo la uzimaji wa mitambo ya kurusha
matangazo ya televisheni kwa njia ya Analojia Bofya play..
Maandalizi ya kuzima mitambo ya analojia ya Utangazaji wa televisheni kwa jiji la Mwanza na vitongoji vyake, yamekamilika kwa kuwashirikisha wadau wa sekta ya utangazaji hapa Mwanza ambapo mitambo hiyo itazimwa usiku wa tarehe 28 Februari 2013.
Elimu kwa umma kupitia mbinu mbalimbali kuhusu mchakato wa kuhamia katika teknolojia ya mfumo wa utangazaji wa digitali imekuwa ikitolewa kwa kiwango cha kuridhisha. Matangazo ya digitali yanawafikia watu asilimia zaidi ya 22% kati ya asilimia 24% ya wanaopata matangazo ya televisheni ya analojia.
Kutoka kulia ni Mabere Makubi, Sita Tuma, .. na Nashon Kennedy. |
Vipi hatma ya simu zinazonasa mawasiliano ya televisheni zikitumia antena zake ndogo hivi, ndiyo tuseme sasa zitageuka kuwa mapambo?
Sikiliza jibu kwa kubofya play...
Serikali ilifikiria kwa kina zoezi zima lakuzima mitambo ya televisheni ya teknolojia kwa makini sana. Ili kufanikisha zoezi hili bila kuwa na usumbufu mkubwa, serikali iliweka ratiba ya uzimaji kama ifuatavyo:-
(1) Dar es salaam- 31 dec 2012; Tayari mitambo imezimwa.
(2) Dodoma & Tanga- 31 jan 2013; Tayari mitambo imeshazimwa.
(3) Mwanza- 28 feb 2013; Zimebaki siku 3 tu!
(4) Moshi & Arusha- 31 march 2013;
(5) Mbeya- 30 April, 2013.
Sehemu ya waandishi wa habari waliohudhuria hii leo kwaajili ya kuuhabarisha umma hatua hiyo ya Mamlaka ya Mawasiliano nchini. |
Serikali inatarajia kupata ushirikiano wa karibu kutoka kwa wadau wa sekta ya utangazaji na wananchi kwa ujumla katika kipindi cha uzimaji wa mitambo ya utangazaji wa televisheni ili kufanikisha zoezi la uzimaji wa mitambo ya utangazaji ya taknolojia ifikapo tarehe 28 Februari 2013.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.