ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, February 5, 2013

YALIYOJIRI AFRIKA KWA PICHA.

Wenyeji wa wilaya ya Chokwe nchini Msumbiji, walilazimika kupanda juu ya paa za nyumba zao pamoja na mali zao siku ya Ijumaa kufuatia mafuriko makubwa katika mto Limpopo. Takriban watu 170,000 wamepoteza makao yao katika wiki mbili zilizopita
Siku ya jumamosi watu waliokuwa abiria wa Ferry katika bandari ya Mombasa, walionekana kushtushwa na lori iliyokuwa inazama baada ya kupoteza mwelekeo kuwagonga abiria waliokuwa ndani ya Ferry  mara baada ya kuchomoka ikiwa haina vigingi kuzuia isitembee. Watu 11 waliuawa papo hapo.
  
Jumanne ,mjini Lagos Nigeria, mwanaume huyu akichoma nyama ijulikanayo kama "suya" kwa lugha ya mtaa. Anawaandalia mashabiki waliofika hapa kujionea mechi ya Nigeria dhidi ya Ethiopia, nje ya uwanja kwenye skrini kubwa. Super Eagles walishinda mabao 2 kwa nunge.

Na hapa mashabiki wa Ivory Coast, wanahakikisha wamevalia kuvutia kabla ya mechi yao dhidi ya Algeria mjini Rustenburg Jumatano. Timu hizo zilienda sare ingawa tayari walikuwa wamejipatia nafasi kwenye robo fainali lakini hatimaye walikuja kubanjuliwa michuanoni na Nigeria 2-1


Jumatano, vijana wa Mali mjini Gao, eneo lililokuwa ngome ya wapiganaji wa kiisilamu ulikombolewa na wanajeshi wa Mali mwishoni mwa wiki , wanajaribu kumzuia mshukiwa wa wizi kutoroka

Hapa ni katika mto mmoja nchini Afrika Kusini siku iliyofuata , mfanyakazi wa shamba hili alilazimika kumkamata mamba huyu aliyetoroka kutoka shamba la kuwahifadhia mamba..
Kwahisani ya bbc swahili.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.