SERIKALI imeingilia suala la uchaguzi wa
Shirikisho la Michezo
nchini Tanzania (TFF) na kuamua kuifuta katiba ya shirikisho hilo inayotumiza
hivi sasa ambayo ilirekebishwa mwaka jana (2012) pamoja na kuagiza ifuatwe katiba ya awali ya mwaka 2006.
Kauli hiyo imetolewa leo na Waziri wa Habari,
Vijana, Utamaduni na
Michezo, Dk. Fenella Mukangara akuzungumza
na wanahabari jijini Dar es Salaam na kuitaka
TFF iitishe Mkutano Mkuu kama inataka kufanya marekebisho
ya Katiba yake.
Katika ufafanuzi wake Dk. Mukangara ameagiza TFF kufuata sheria na Kanuni za Baraza la Michezo Tanzania (BMT) ikiwa inataka kufanya marekebisho ya katiba yake. "Naelekeza na ifahamike kuwa hakuna chama chochote cha michezo nchini kilicho juu ya BMT. TFF wafanye uchaguzi wa viongozi kwa mujibu wa Katiba ya TFF ya mwaka 2006 kwa kuzingatia sheria na kanuni za baraza la michezo la Taifa," alisema Dk. Mukangara.
Akifafanua zaidi Dk. Mukangara alisema baada ya wataala kupewa kazi yakuangalia mchakato wa mabadiliko ya katiba ya TFF na mgogoro wa uchaguzi unaoendelea, wizara imebaini; sheria Na. 12 ya BMT na marekebisho yake Na. 6 ya mwaka 1971, pamoja na kanuni za BMT za usajili Na. 442 za mwaka 1999 zimekiukwa.
"...Ha kanuni ya BMT Na. 11(1) inayoeleza wazi utaratibu wa marekebisho ya katiba; 'haukufuatwa'. Kimsingi TFF walitakiwa wajaze fomu Na. 6, 7, 8 na 9 kwa mujibu wa sheria na kanuni za BMT. Sasa TFF hawakufuata taratibu nilizozielekeza kwa mujibu wa sheria na kanuni za BMT," alisema Waziri huyo mwenye dhamana ya Michezo Tanzania.
Aidha Serikali imeitaka TFF na Msajili wa Michezo Tanzania kuwajulisha FIFA ambao walikuwa wameingilia mgogoro huo uamuzi uliofikiwa na Serikali ili nao wajue kinachoendelea kwa sasa.
*Imeandaliwa na www.thehabari.com
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenella Mukangara |

Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.