ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, January 18, 2013

WAWEKEZAJI SERENGETI BALLON WAWANYASWA WATANZANIA

 Na Shomari Binda
          Serengeti,


WAFANYAKAZI Watanzania wa Kampuni ya Serengeti Balloon Safaris inayofanya shughuli za Kitalii katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti wamelalamikia Uongozi wa Kampuni hiyo kwa kuwafanyisha kazi kwa zaidi ya miaka 10 bila kuwapa mikataba inayotambulika Kisheria licha ya kufatilia suala hilo katika ngazi zinazohusika.

Wakizungumza na Waandishi wa Habari Mjini Mugumu,Wafanyakazi hao  walisema wanashangaa kuona Wawekezaji wa Kampuni hiyo kutoka Nchini Uingereza ambayo Meneja anayesimamia shughuli zao ni mzawa kushindwa kuwatimizia masharti ya kazi huku wakiwatolea lugha zisizo za kiungwana wanapofatilia mikataba yao.

Walisema licha ya kufatilia kwa muda mrefu suala la kutengenezewa mikataba ya Kisheria kwa Meneja wa Kampuni hiyo waliyemtaja kwa jina la Maria Straus licha ya kuwa ni Mtanzania mwenzao ameshindwa kuwasaidia na kila anapoitwa katika vikao vya kulizumzia suala la mikataba amekuwa akishindwa kufika bila kutoa sababu zozote.

"Tunashangaa kuoa Mtanzania mwenzetu kushindwa kua karibu na suala hili huku akijua ni muda mrefu tunafanya kazi bila kuwa na mikataba ya Kisheria ambayo itaweza kutulinda katika shughuli hizi za Utalii ambazo tunazifanya katika mazingira ambayo pia ni hatari kwa maisha yetu. 

"Kabla ya kuja hapa kwenye Kampuni ya Balloon alikuwa ni Meneja wa Kampuni nyingine ya Utalii ya Abercombie and Kent (A & K) nako amekuwa na matatizo kama haya ya kutokuwathamini Watanzania wenzake na kupelekea kufutwa kazi baada ya kukataliwa na Wafanyakazi,walisema wafanyakazi hao.

Walidai kuwa wamepanga kufanya mgomo ndani ya mwezi huu wa kutofanya kazi kwa muda usiojulikana katika vituo vyote vya Seronera,Ndutu,Kirawira na Sasakwa kitu ambacho kitakuwa ni aibu kwa Taifa na wageni wanaofanya Utalii wa Balloon kutokana na Mtalii mmoja kutoa Dolla 499 kwa safari moja.

Madai ya Wafanyakazi hao licha ya kutaka mikataba ya Kisheria pia wanalalamikia nyongeza ya mishahara kutokana na mishahara inayotolewa na kampuni kutokukidhi mahitaji kutokana na kutolewa mshahara wa shilingi laki moja na themanini 180,000 kwa kima cha chini kiwango ambacho walidai ni kidogo kuliko ya kile walichokuwa wakilipwa mwanzoni.

Wafanyakazi hao walidai kuwa baada ya kuona Meneja wao anashindwa kulifatilia suala lao waliamua kulifikisha katika Ofisi za Chama cha Wafanyakazi wa Mahotelini (CHODAWU) Mkoa wa Mara tangu mwezi wa 8 mwaka jana kwa ajili ya ufatiliaji zaidi na kuamua kuwabana wawekezaji na kuwataka kuandaa mikataba ya Kisheria.

"Tumefika (CHODAWU) na wao walikaa na Wawekezaji kupitia Mwanasheria wao katika kuandaa mikataba na tulipoletewa tuliona bado inamapungufu kutokana na vipengele mbalimbali na kushindwa kuijaza na wao tumesikia wamepeleka CHODAWU tena kwa kweli suala hili bado linatusumbua kutokana na kulifatilia kwa muda mrefu,"walisema.

Akizungumzia suala hilo Katibu wa (CHODAWU) Mkoa wa Mara Daudi Mapuga alidai kulipokea suala hilo katika Ofisi yake na wanalishughulikia ili yale yanayodaiwa na Wafanyakazi hao yaweze kushughulikiwa kwa mujibu wa kanuni za kazi na mikataba ya Kisheria inavyoeleza.

"Ni kweli nimepokea suala la wafanyakazi wa Serengeti Ballon Safaris wakitaka mikataba ya Kisheria kutoka kwa waajili,tumekaa na waajili pamoja na Mwanasheria wao na tumekubaliana vipengele mbalimbali naamini baaadaya kuvikamilisha tutaenda kukutana na Wafanyakazi kwa ajili ya kuisaini kwa mujibu wa Sheria,"alisema Mapuga.

Akizungumzia suala la Wafanyakazi hao,Mbunge wa Jimbo la Serengeti Stiven Kebwe alisema hakuna Sheria yoyote inayotaka Wawekezaji kuwanyanyasa Watanzania katika shughuli yoyote na kuwataka waajili wa Baloon kuhakikisha wanalifanyia kazi suala la kuandaa mikataba sahihi ya Kisheria ambayo inakidhi mahitaji na hali halisi.

Kebwe alisema Sheria ya mikataba lazima izingatiwe na mamlaka zinazohusika lazima zifanye ufatiliaji kwa kuwa ameshapokea malalamiko mengi kutoka katika kampuni mbalimbali za Utalii katika Hifadhi ya Serengeti ambayo pia ni sehemu ya Jimbo lake analo liongoza.  

"Haiwezekani kuendelea kuangalia na kulikalia kimya suala la Watanzania kuendelea kunyanyaswa na Wawekezaji kutokana na maslahi na kufanya kazi bila mikataba sababu si busara Mtalii kuruka na Balloon mara moja  na kutoa Dolla 499 huku mfanyakazi mzawa anayefanya anayefanya kazi kubwa akilipwa shilingi laki moja na themanini,"alisema Kebwe.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.