Na ALBERT G. SENGO: MAGU
HALMASHAURI ya Wilaya ya Magu Mkoa wa Mwanza imeanza kutekeleza zoezi
la kuwauwa Mbwa wazururaji wasiyo kuwa na makazi ya kudumu na kumilikiwa na
watu ili kuzuia kuenea kwa kichaa cha mbwa Wilayani humo.
Hatua hiyo inatokana na Wilaya hiyo kuwa na idadi
kubwa ya mbwa wapatao 12,500 ambapo wengi wao hawana makazi maalumu na wamekuwa
wakizaagaa hovyo na kukumbwa na ugonjwa wa ngozi na kichaa cha mbwa na
kusababisha kuwauma watu na kuwaambukiza virusi vya kichaa cha mbwa jambo ambalo
limekuwa likisababisha vifo na usumbufu kwa wanaoumwa kupelekwa umbali mrefu
kupatiwa tiba .
Daktari wa Mifugo wa Wilaya ya Magu Bw.Faustine
Msoke ambaye pia ni Kaimu Afisa Mifugo na Kilimo wa Halmashauri ya Wilaya ya
Magu amesema kuwa tayari kampeni hiyo imeanza kutekelezwa na kuwezesha kuuawa kwa
mbwa wapatao 10 kwa kupigwa risasi katika kijiji cha Kitongosima kilichopo Kata
ya Lugeye Wilayani humo.
Bw.Msoke amesema kuwa zoezi la kampeni hiyo maalumu litatekelezwa
katika maeneo ya kata tatu ambayo yameonekana kuwa na mbwa wengi wanaozurura
bila kuwa na makazi maalumu na kumilikiwa na wafugaji katika kijiji cha Kitongo
sima Kata ya Lugeye,Kijiji cha Masanza kona Kata ya Kiloleli na Kata ya Magu
mjini katika mitaa ya Itumbili na Nyalikungu.
“Mbwa wa aliyepata kichaa ni hatari sana kwa
binadamu na wamekuwa wakiuma watu hovyo jambo ambalo husababisha kuambukiza
virusi vya kichaa cha mbwa pale anapomuuma Binadamu na husababisha mgonjwa
aliyeumwa na mbwa wa kichaa kuhitaji Tiba haraka na Chanjo ambayo inapatikana
tu kwenye Hospitali ya Wilaya ya Magu hali ambayo ni usumbufu kwa wananchi wa
maeneo ya vijijini kuhitaji kusafiri umbali mrefu kwenda kutafuta matibabu
hayo”alisema Dkt.Msoke.
Ametowa wito kwa wafugaji wa mbwa kuwapenda umbwa
wao na kuwadhibiti kwa kutowaruhusu kutembea hovyo mitaani na kufuata taratibu
za kuwafungulia saa 1:00 usiku na kuwafungia saa 12:00 alfajiri kila siku ili
kuepuka kukumbwa na ugonjwa wa kichaa cha mbwa na ngozi pamoja na kuuawa katika
kampeni ya kuuwawa mbwa wazururaji.
Baada ya zoezi la kuwauwa mbwa wazururaji kumalizika
na kubaki mbwa wanaomilikiwa na wafugaji kukamilika halmashauri hiyo imeandaa
chanjo kwa ili kuepuka ugonjwa wa ngozi na kichaa cha mbwa.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.