WAZIRI wa Afya wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar Juma Duni Haji (CUF) amesema kuwa Serikali ya Tanzania haina budi kuketi chini na kujitathimini ili kukabiliana na tatizo la vurugu za Mtwara.
Duni ameongeza kuwa wananchi wa Mtwara wanategemea zao la Korosho tu huku Bandari ya Mtwara ikiwa imetelekezwa na hakuna juhudi zilizochukuliwa kuijenga, nazo barabara zikiendelea kuwa mbovu kwani tangu uhuru na sasa ni miaka 52 mkoa wa Mtwara unaendelea kuwa nyuma kiuchumi na kimaendeleo hivyo
hakuna budi kutatua yale yanayo ikabili mikoa hiyo ya kusini ndipo uvunaji wa gesi ufanyike.
“Mkiona mtawala anaanza kutumia risasi na mabomu hizo ni dalili za kushindwa hoja, na hili si jambo jema serikali inatakiwa kujibu hoja na si kutumia vyombo vyake
vya dola kuuwa kwa kutumia risasi za moto hivyo wananchi wajiandae watakufa
sana kwa kuwa serikali haitaki suruhu na wananchi wake hivyo ikataeni CCM” alisema.
Duni amekinyooshea kidole Chama cha Mapinduzi (CCM) kwani tangu kupata uhuru kilipounda serikali kimeshindwa kutoa Elimu yenye ubora na matibabu kwa wanawake wajawazito bure kama ilivyofanywa na serikali ya umoja wa kitaifa Zanzibar hivyo wananchi wasikichague chama hicho kwa mwaka 2015 kuunda tena serikali huku pia akiwataka CHADEMA kuacha kujiita kuwa Chama kikuu cha upinzani kwa vile hakiungwi mkono Zanzibar hivyo hakitaweza kushika dola .
Kwa upande wake Mbunge wa viti maalum CUF, Mkiwa adam Kimwanga amewaasa wananchi hasa vijana wasikubali kutumiwa na wanasiasa kwani tangu
vijana watano waliodaiwa kuwa wafuasi wa CHADEMA waliokamatwa kwa tukio la
kuchoma moto ofisi za CCM Kata za Isamilo na kuhukumiwa kwenda jela miaka 15
hakuna hata kiongozi na wabunge wa CHADEMA wanaowakumbuka hata kuwapelekea
sabuni huko Gereza la Butimba. Msikilize zaidi hapo juu.
Mjumbe wa Baraza Kuu la CUF ambaye pia ni diwani wa kata ya Lyoma jimbo la Sumve wilaya ya Kwimba Julius Samamba, akihutubia mkutano huo. |
Sehemu ya wananchi waliojitokeza kiwanjani hapa. |
Wananchi kusanyikoni. |
Tafakari kwa kina na usikivu. |
Safu iliyosheheni akinamama kusanyikoni hapo. |
Waziri wa Afya wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar Juma Duni Haji akizungumza na waandishi wa habari kwa masuala ya ufafanuzi. |
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.