Bw. Samson Chacha Boroyi |
KADA wa CHADEMA Bw. Samson Chacha Boroyi ambaye ni Mjumbe wa Kamati Tendaji ya Baraza la Vijana la Chadema (BAVICHA) Wilayani Ilemela Mkoani Mwanza, amejiengua katika chama hicho huku akikiponda chama hicho kuwa kinaongoza nchini kwa kuwafanya watu Chambo na kuongozwa kwa maslahi ya Ukanda .
Akizungumza na
vyombo vya habari Jijini Mwanza amewataja waziwazi baadhi ya viongozi wa
CHADEMA wakiwemo wale wa Kitaifa kuwa hawataki kutii Sheria, Kanuni na Taratibu
za nchi hivyo siku wakipatiwa Dola, hali itakuwa mbaya kuliko ya Misri na Libya.
Mwalimu Samson Boroyi ameyasema hayo huku akikiita Chama
hicho kuwa ni Kampuni ya kundi dogo la vigogo wa Kanda ya Kaskazini japokuwa
wamekuwa wakijinadi kuwa ni Taasisi ya Kisiasa, alidai kwamba viongozi wa Chama
hicho wakiwemo Katibu Mkuu Dkt Willbroard Slaa wamekuwa wakiitumia CHADEMA
vibaya kwa kushindwa kufuata Katiba yake na hata kuwa watu wasiotii sheria za
Nchi na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Msikilize Bofya play..
Bw.Boroyi ambaye pia alikuwa Katibu Mwenezi wa Chadema Kata ya Nyamanoro wilayani Ilemela, alieleza kwamba pamoja na chama hicho kuendeshwa kama kampuni ya mtu binafsi, kundi hilo dogo ndilo linalotoa maamzi bila kuzingatia Katiba yake na maslahi ya wengi.
Ameongeza kuwa hata Bw Wenje alitoa ahadi ambayo ameshindwa kuitekeleza tangu aitangaze kwenye mikutano yake ya hadhara na kujigamba kusomesha watoto 1,960 katika Sekondari za Kata na kuzipatia madawati, kuboresha huduma ya Hospitali ya wilaya ya Nyamagana ya Butimba wakati hali ni kinyume na mbwembwe hizo. Msikilize Bofya play..
Hata hivyo Bw.Boroyi
hakuwa tayari kutaja chama atakachojiunga nacho hadi hapo baada ya wiki mbili,atakapokuwa
ametafakari kwa kina ni Chama kipi bora atakachojiunga nacho ili asikosee tena
kama alivyopotea muda wake kujiunga na
Chadema toka mwaka 2007akiwa mwanachama hai kwa Kadi namba 0359614 na kuahidi
kuirejesha Kadi hiyo kwa Katibu wa Wilaya ya Ilemela Jumatatu ijayo ili
kuthibitisha kukiacha kabisa chama hicho.
Tuko mbioni kusikiliza upande wa pili.
Tuko mbioni kusikiliza upande wa pili.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.