TAARIFA KW AVYOMBO VYA HABARI
TAREHE 27/12/2012
Shirilisho la Ngumi la Kimataifa (IBF)
limepongeza bingwa mpya wa uzito wa Super Middle katika bara la Afrika, Ghuba
ya Uajemi na Mashariki yaa Kati, Mtanzania Francis Cheka.
Katika barua yake aliyomtumia Francis
Cheka ya tarehe 28/12/2012 Mwenyekiti wa kamati ya Ubingwa wa IBF/USBA Lindsey
Tucker alisema "Tunachukua fursa hii kukutakia maisha na mafanikio
mazuri kama bingwa wa IBF na kumhimiza kuishi kama bingwa". Cheka
atatakiwa kutetea taji lake katika kipindi cha miezi sita kufikia mwezi wa 6
mwakani dhidi ya mpinzani ambaye ana rekodi ya mapambano yasiyopungua 15 na
mengi awe ameyashinda hususan mapambano mawili ya mwisho.
Aidha IBF inampongeza bondia Chiotcha
Chimwemwe kutoka Malawi kwa ushupavu wake na ushindani mzuri katika pambano
hilo lililofanyika katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid katika jiji la Arusha
tarehe 26 Desemba, 2012.
Imetolewa na:
Onesmo A.M. Ngowi
Rais
IBF/USBA Afrka, Ghuba ya Uajemi an
Mashariki ya Kati
CHIOTCHA AONJA MACHUNGU YA CHEKA
Bondia kutoka Jamhuri ya watu wa Malawi
Chiotcha Chimwemwe alionja machungu ya Mtanzania Francis Cheka katika mpambano
wao uliopewa jina na “Vita vya Ziwa Nyasa” tarehe 26 Desemba 2012 siku ya
Boxing Day jijini Arusha.
Ulikuwa ni mpambano wa mwaka ambao bondia Francis Cheka nusura aupoteze katika raundi ya pili wakati konde zito la kushoto la kapteni Usu kutoka katika jeshi la jamhuri ya watu wa Malawi, Chiotcha lilipompeleka chini na kuinuka kwa msaaada wa kamba za ulingo.
Francis Cheka. |
Konde hilo zito lilifungua mpasuko
mkubwa katika paji la Cheka na hivyo kuleta wasiwasi kwa mashabiki zaidi ya
elfu 10 waliofurika katika uwanja wa Sheikh Amri Abed kumshughudia Cheka
akipambana kiume kwelikweli.
Raundi ya kwanza mpaka ya nne Chiotcha
alikuwa anamiliki mpambano huo na makonde mazito ya mkono wake wa kushoto kwani
anatumia staili ya South Paw inayomlazimu kutanguliza mbele mguu wa kulia.
Ni katika raundi ya sita ambako Cheka
aliweza kubadilisha mwelekeo wa mpambano kwa kuanza kumwadhibu Chiotcha na
makonde mazito ya kombinasheni yaliyomfanya Mmalawi huyo kumkumbatia bila
mafanikio Mtanzania huyo asiyepigika.
Cheka aliwanyanyua mashabiki waliojaa
uwanjani wakiongozwa na Mstahiki Meya wa jiji la Arusha, Mh. Gaudence Lyimo
alipompiga bila huruma Chiotcha na kumlazimu refarii wa kimataifa wa mpambano
huo Nemes Kavishe wa Tanzania kumwonya kutomshika Cheka kama vile anapigana
mieleka.,
Juhudi za Chiotcha kujisalimisha kwa
kumkumbatia Cheka hazikuzaa matunda kwani aliendelea kupewa mkong’oto na mwana
huyo wa Kitanzania aliyejizolea sifa kemkem kwa kuwapiga wapinzani wake.
Mashabiki wengi walinyanyuka katika
viti vyao katika raundi ya 12 ya lala salama wakati Cheka alipodhihirisha kweli
ni bondia asiyepigika kwa kumpiga makonde mazito kichwani Chiotcha na kumfanya
apepesuke kila mara.
Katika mchezo huo ulioandaliwa na
kampuni ya Green Hills (T) Investment ya jijini Dar-Es-Salaam inayomilikiwa na
bingwa wa zamani wa taifa Andrew George, mabondia wa mapambano ya utanguliizi
walikuwa wa ngumi za ridhaa kutoka katika jiji la Arusha.
Mpambano huo ulisimamiwa na Rais wa IBF
katika bara la Afrika, Ghuba ya Uajemi na Mashariki ya Kati, Mtanzania Onesmo
Ngowi akisaidiwa na Kamishna wa TPBC kutoka Jiji la Arusha bw. Roman Chuwa.
Refarii alikuwa Nemes Kavishe kutoka
Tanzania wakati majaji walikuwa: Daudi Chikwanje kutoka Malawi, Boniface
Wambura kutoka Tanzania na Galous Ligongo kutoka Tanzania.
Imetolewa na
Uongozi, TPBC
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.