Na Albert G. Sengo.
KOCHA wa Timu ya Taifa Stars Kim Poulsen ameusifia uwanja wa CCM kirumba na kusema kwamba ni moja ya viwanja bora nchini na
wachezaji wake watautumia vyema kuibuka na ushindi dhidi ya Harambee Star ya
Kenya watakaocheza nao kwenye dimba hilo siku ya Jumatano ukiwa ni mchezo wa
kirafiki wa kimataifa kuendana na kalenda ya FIFA uliopangwa kufanyika Mkoani
Mwanza na shirikisho la mpira wa miguu nchini TFF.
Akizungumza baada ya mazoezi ya timu hiyo kwenye
uwanja wa CCM Kirumba asubuhi ya leo kocha huyo ameeleza kuwa mchezo wa Taifa Stars na
Harambee Star utakuwa mgumu kulingana na kila timu kujianda na maandalizi ya
mchezo huo huku ikizingatiwa kuwa wapinzani wao Harambee star imeshusha wachezaji wake tegemeo wanaosukuma kandanda nchi za Ulaya kufanya upinzani mkali sanjali na ujio wa Mbwana Samata na Thomas Ulimwengu wanaokiputa TP Mazembe hali iliyoongeza molali kwa wachezaji wake .
Poulsen amesema kuwa baada ya mchezo wa jumatano
timu hiyo ya taifa itaendelea na kambi yake Jijini Mwanza kujiandaa na michuano
ya Challenge Cup inayotarajia kuanza hivi karibuni nchini Uganda kwa
kushirikisha Mataifa ya nchi za Ukanda wa Afrika mashariki na kati zitachuana .
Wachezaji wote wanamolali na wanaonekana
kushirikiana vyema na nidhamu kwenye kambi ni nzuri na matumaini ya kushinda mchezo huo kutokana na
ushirikiano ulionyeshwa na vionozi wa chama cha mpira wa miguu Mkoa wa Mwanza
(MZFA),TFF na wadau wengine wa michezo kuanzia mapokezi na ubora wa Kambi ya
timu iliyopo katika Hoteli ya La-Kairo umewapa matumaini wachezaji kufanya
vizuri na kucheza kufa na kupona ili kuibuka na ushindi wa mechi hiyo ya
kimataifa.
Nahodha wa Stars Juma Kaseja akizungumzia kambi na
mazoezi ya timu hiyo Jijini Mwanza amesema kuwa wachezaji wamefurahia mapokezi
na mazoezi yanaonyesha kila mchezaji na molali ukizingatia wote ni wachezaji
waliochaguliwa kutoka timu zinazoshiriki Ligi kuu ya Vodacom hivyo ni wazuri
kilichobaki ni mwalimu kuwaaunganisha kucheza kwa mfumo atakaoutumia jumatano.
Kaseja ameongeza kuwa wachezaji wote wanatambua
wajibu wao hivyo kila mchezaji ametambua thamani yake ya kuchaguliwa kuchezea
timu ya taifa hivyo jukumu kubwa ni kuitumikia timu hii kwa moyo na uzalendo
kwavile ni timu ya watanzania wote hivyo kufanya vizuri kwa timu hii pia
kutatuongezea alama FIFA kwa vile ni mchezo wa kimataifa wa kirafiki
tunawaahidi watanzania kuwa hatutawaangusha bali wajitokeze kwa wingi kuja
kutushangilia ndani ya dimba la CCM Kirumba Jumatano na kwamba Harambee
hawatatoka na ushindi.
MWISHO.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.