Hatua hiyo ya kukamatwa inafuatia madiwani hao na voiongozi kudharau wito wa mahakama na oda yakuwataka kusitisha zoezi la kumchagua mgombea wa nafasi ya Meya na Naibu meya wa Manispaa ya Ilemela kupitia tiketi ya CHADEMA kutokana na wanachama ambao ni madiwani kupibga kuvuliwa uanachama na Kamati kuu ya chama hicho taifa.
Kesi hiyo ya kupinga kuvuliwa uanachama ilifunguliwa na diwani wa kata ya Kitangili Henry Matata (CHADEMA) na diwani wa kata ya Igoma Adam Chagulani (CHADEMA) ambao walivuliwa uanachama na Kamati kuu ya CHADEMA nao kupinga katika mahakama, hivyo shauri lililopo Mahakamani hapo chini ya Hakimu Mfawidhi Angelo Lumisha ilikitaka chama hicho kusitisha shughuli zote za uchaguzi wa nafasi ya Meya na Naibu wake mpaka pale kesi iliyopo mahakamani hapo itakapotolewa maamuzi.
Hata hivyo viongozi hao wa wilaya walionekana kukaidi agizo hilo la Mahakama ikiwemo madiwani hao ambapo leo walitakiwa kufika mahakamani hapo baada ya wito wa zaidi ya mara mbili ili kuielezea mahakama kwa nini wamekaidi kutekeleza amri halali ya mahakama kwa kuendelea na zoezi la Uchaguzi wa nafasi za Meya na Naibu wake ndani ya chama hicho huku wakitambua kuwa mahakama ilisitisha kwa kutoa maelekezo kupitia oda halali.
Akisoma uamuzi wa mahakama hiyo hakimu mfawidhi wa mahakama hiyo Mhe. Lumisha imetengua wagombea ambao walikuwa wamechaguliwa na chama hicho kuwania nafasi hizo, Nafasi ya Meya alichaguliwa Bw. Aboubakari Kapela diwani wa kata ya Nyamanoro na naibu Meya alichaguliwa Bw. Bahati Kahungu wa kata ya Kirumba hadi hapo kesi ya msingi itakapo amriwa na si vinginevyo.
Waliowekwa mahabusu ni Josephat Manyerere (diwani kata ya Nyakato), Bahati Kahungu (diwani kata ya Kirumba) na Carlos Majura (Katibu Mwenezi) wote kutoka CHADEMA huku katibu wa wilaya akitafutwa kukamatwa ili kuunganishwa na wenzake ili kutolewa hukumu na hakimu mfawizi kwa kosa la kudharau amri halali ya mahakama hiyo hivyo waliokamatwa wakiamriwa kupelekwa mahabusu Gereza la Butimba na kunyimwa dhamana hadi hapo atakapopatikana Katibu wa Wilaya Bw. John Anajus.
HABARI KAMILI TUTAENDELEA KUWAPATIA....
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.