ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Sunday, September 16, 2012

UMOJA WA WANAWAKE KWEA WAKUTANA NA WAZIRI MKUU NA MKEWE, WACHANGISHA FEDHA KUTUNISHA MFUKO WAO, HALMASHAURI YA JIJI LA MWANZA YAUPIGA JEKI KWA KUTOA AHADI YA KIWANJA.

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akiwasili New Mwanza kwaajili ya kushiriki chakula cha jioni kilichoandaliwa na Umoja wa akinamama wenye fani tofauti tofauti jijini Mwanza KWEA wenye lengo la kuimarishana kiuchumi.  


Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mizengo Pinda akitoa neno la shukurani kwa Umoja wa akinamama KWEA.


Wanachama wa Kwea katika meza ya Itifaki wakiweka mambo sawa akina mama hawa wamenuia kuutanua Umoja huo ili upate kufika maeneo yote nchini Tanzania.


Mlezi wa Umoja huo Mh. Gachuma (MNEC) akitoa angalizo kwa wana KWEA ili kuujenga na upate mafanikio, mbali na kauli thabiti aliyoitoa pia alishiriki kufanikisha harambee isiyokuwa rasmi ambayo ilifanyika usiku huo wa chakula cha jioni.


Mke wa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Tunu Pinda ambaye ndiye alikuwa mgeni rasmi usiku huo akizungumza na akina mama wa KWEA huku akisifia ujasiri wa akinanama hao kuthubutu kutambulisha kitu kipya kwenye jamii ya watanzania kwa imani ya kuwezeshana kutokana na kipaji cha kila mama mshiriki. 


Mkuu wa mkoa wa Mwanza Evarist Ndikilo akizungumza kwenye hafla hiyo ya KWEA.
"Ni vyema ili KWEA iendelee kukwea na kupaa juu kimafanikio, ni lazima utendaji wenu wa kila siku uendane na madhumuni ya uanzishwaji wa Umoja wenu, mkikiuka na kila mtu aende kivyake kwa matakwa yake ni wazi kuwa hamtadumu"


Moja kati ya meza za wana KWEA Mwanza.


Mwenyekiti wa UWT wilaya ya Nyamagana na Diwani wa viti maalum (CCM) Mhe. Sikitu Sanziyote akisalimiana na mgeni rasmi mama Tunu Pinda.


Mbunge wa Bariadi Magharibi Mh. Andrew Chenge akizungumza na kusanyiko hilo lililoalikwa kupata chakula cha jioni ambapo naye alishiriki kuchangia mfuko wa KWEA ili kuuboresha.


Wadau kusanyikoni.


Mkurugenzi wa jiji la Mwanza Bw. Wilson Kabwe akitoa ahadi mbele ya waziri mkuu kwa ofisi yake kuhakikisha inatenga eneo maalum la kiwanja kwa ajili ya Umoja huo kujenga ofisi zake ili kuboresha utandazaji huduma mbalimbali zilizokusudiwa katika kumkwamua na kumwinua mwanamke nchini.


Shangwe zililipuka mara baada ya kwa kauli ya mkurugenzi wa jiji Bw. Wilson Kabwe kuainisha jinsi ofisi za Halmashauri ya jiji la Mwanza zitakavyoshiriki kufanikisha Umoja wa KWEA kupata kiwanja kwaajili ya kujenga ofisi zake zitakazo kuwa zikitoa huduma mbalimbali sanjari na uwekezaji.


Waalikwa mbalimbali wamehudhuria tukio hilo.


Neno la shukurani kutoka kwa Uongozi wa KWEA lililowasilishwa na Bi. Shufaa.


KWEA


Picha ya pamoja.



Kwa umakiiini...


Meza zilipendeza


Usiku wa chakula maalum.


Zawadi toka kwa umoja wa KWEA Kwenda kwa  Mke wa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Tunu Pinda ambaye ndiye alikuwa mgeni rasmi usiku huo.


Zawadi toka kwa umoja wa KWEA Kwenda kwa  Mh. Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Peter Pinda.


Picha ya pamoja kutoka kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Kondisaga almaarufu kwa jina 'Mtumishi wa Mungu', pamoja na G. Sengo (katikati) na mwenyeji wetu Mwenyekiti wa Kamati ya Halmashauri kuu ya Taifa CCM Mh. Christopher Gachuma. 
Umoja wa KWEA ukiagana na Mh. Waziri Mkuu Pinda ndani ya New Mwanza Hotel.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.