ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, September 6, 2012

ROLI LA SHEHENA YA SABUNI LATEKETEA MISUNGWI MWANZA

Kushoto ni Inspector Meena ambaye ni OC Trafficking wa wilaya ya Misungwi. Ni gari (roli) lililokuwa limebeba shehena ya sabuni likitokea jijini Dar es salaam kuelekea Mwanza lilipofika eneo la kati  hatua chache kutoka  Misungwi mjini hitilafu ikatokea hii ni kupitia msuguano wa matairi ukasababisha matairi kupata moto na hatimaye moto mkubwa ukazuka na kusambaa sehemu nyingine ukichagizwa na upepo wa mwendo kasi wa gari na kuwa balaa.

Kwa mujibu wa Inspector Meena ambaye ni OC Trafficking wa wilaya ya Misungwi ambaye aliyekuwa eneo la tukio amesema kuwa taarifa ya kutokea kwa ajali hiyo ya moto waliipata kupitia kwa dereva wa gari  hilo ambaye alithibitisha na kutoa mwongozo wa eneo husika, hakuna aliyejeruhiwa wala kifo kilichotokea.

Shehena ya sabuni iliyoteketea na moto...Polisi walifika kwenye eneo la tukio haraka nao wakawasiliana na zimamoto Mwanza ambao nao walifika eneo la tukio na kufanikiwa kuudhibiti moto huo.

Tairi zilizosuguana na kusababisha moto chanzo cha ajali hiyo.

Ni roli lenye namba za usajili T 476 BBA lenye tela mbili zenye namba T 505 BBA.

Ukusanyaji wa sabuni zilizo kuwa na japo afadhali ukiendelea kwa msaada wa wanakijiji.

Hizi ni baadhi ya mali zilizo na afadhali.

Eneo la tukio.


Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.