Licha ya kupokea barua ya kutoruhusiwa kufanya maandamano toka Jeshi la polisi Mwanza, Waandishi wa habari mkoa hapa hatimaye leo wameandamana na kufanikisha azma yao yaani kuungana na waandishi wengine hapa nchini kufikisha ujumbe kwa serikali na jeshi la polisi kulaani mauaji ya kikatili ya Mwanahabari mwenzao wa kituo cha televisheni cha Channel Ten mkoani Iringa, Daud Mwangosi aliyeuawa mikononi mwa polisi.
Chama cha waandishi wa habari mkoani Mwanza (MPC) jana jioni kilipokea barua toka jeshi la polisi ikisema kuwa kutokana na kuwa na ugeni wa Waziri mkuu kuanzia tarehe 11/09/2012 hadi tarehe 14/09/2012 ambao unahitaji askari wengi jeshi hilo mkoa wa Mwanza halitakuwa na askari wa kuongoza maandamano ya waandishi wa habari hivyo kuyataka maandamano hayo kupangwa siku nyingine jambo ambalo liliwekwa kwenye mizani na hatimaye waandishi hao wakaja na kauli moja KUENDELEA NA MAANDAMANO.
Maandamano yalifanyika kimya kimya, huku waandamanaji hao wakiwa katika mavazi meusi ya majonzi na vitambaa vyeusi mkononi, midomoni wakiwa wameweka plasta kuashiria ukimya wakapita barabara za mchoro wa maandamano na hatimaye kuishia uwanja wa Nyamagana jijini Mwanza.
Tupe maoni yako
Hv kwel bado 2naendelea kuamini kua nchi hii ina amani wakat wale wanaoleta aman ndo wanatuua tena kikatili vile...! nasubir kwa ham kubwa matokeo ya tume iliyoundwa kuchunguza yale mauwaji ya kikatili vile na pia ni kwanin watu wafe wakat wa mikutano ya chadema tu
ReplyDelete