ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, August 6, 2012

SAFARI KUINUA VIPAJI JIJINI MWANZA IMEANZA

Mkurugenzi wa The Great Lake Zone Entertainment Fabian Fanuel akizungumza na wanachama wa kundi hilo juu ya mikakati mbalimbali iliyowekwa kwaajili ya harakati za kuwakwamua vijana kupitia sanaa na vipaji walivyonavyo kikao kilichofanyika leo katika ukumbi wa Mtema B, Nyakato jijini Mwanza. 

Mkurugenzi Mtendaji  wa The Great Lake Zone Entertainment Mr. Tumaini Ngowi ambaye ametoa mchango mkubwa sana kwa kampuni hii, akitoa mwongozo na kujibu maswali yaliyoulizwa na wasanii mbalimbali waliohudhuria kikao hicho hali kadhalika bw. Ngowi alitumia nafasi hiyo kutoa ushauri, msimamo na dira ya kampuni hiyo ambayo imeanzishwa kwa nia ya kuifanya sanaa ya vijana wa kanda ya ziwa kama ajira rasmi. 

Ni vijana wenye vipaji mbalimbali kutoka wilaya za Nyamagana na Ilemela walio wamehudhuria kikao hiki  mfano Filamu, mitindo, Dancers, Muziki (Bongo Fleva/Gospel), Sarakasi, Ngoma, Komedia Mpira /miguu/basketi/netiball 

The Great Lake Zone Entertainment inajihusisha na masuala mbalimbali ikiwa ni pamoja na Uandaaji wa Matamasha ya Muziki wa aina zote, uibuaji vipaji mbalimbali kwa vijana na jamii, Uandaaji wa mabonanza, Uandaaji wa Semina kwa vijana katika kutoa mwanga na elimu pia.

Kwa umakini zaidi kusanyikoni....

Wananchi wenzangu hizi ni hazina zilizopo kundini.

"Vijana tunasadikika na kuaminika sana katika harakati za kuleta mabadiliko, Hakuna safari iliyofanikiwa kwa jambo lolote linaloonekana Kubwa leo bila kuwa na changamoto, changamoto ni sehemu ya safari ya mafanikio hivyo tusikate tamaa " Meneja wa The Great Lake Zone Entertainment Albert G. Sengo 

Kwa umakiiini wadau wakisikiliza kinachoendelea kusanyikoni..


Mwembwe pia 'zinanhuuuu'
Wito umetolewa kwa makampuni, watu binafsi, mashirika ya dini, wanasiasa, wanaharakati na taasisi mbalimbali nchini kujitokeza kuwekeza ndani ya himaya ya sanaa na vipaji ya The Great Lake Zone Entertainment kwani  ndipo mahala penye ufunguo wa mwanga wa uwezeshaji kanda ya ziwa kwa mawasiliano zaidi tuwasiliane kupitia namba hapo juu ya Blogu hii.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.