ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, August 9, 2012

WAKATI PAMBA QUEENS WAKITAWAZWA KUWA MABINGWA NETIBOLI NYAMAGANA, MTEKATEKA KUZIWEZESHA TIMU SITA ZILIZOINGIA ROBO FAINALI

Licha ya kuahidi kuyaboresha zaidi mashindano hayo mwakani kwa vifaa bora vya kimichezo na nyenzo mbalimbali, Mhasibu mkuu wa jeshi la Polisi mkoa wa Mwanza Noel Mtekateka jana kupitia fainali za mpira wa pete (Netiboli) kwa wilaya ya Nyamagana ameahidi kuwa ataziwezesha timu zote sita zilizo ingia hatua ya robo fainali kwa kuzipatia shilingi laki moja moja kwa kila timu kama sehemu ya zawadi ili kuwapa changamoto washiriki kuwa na mapenzi kwa mchezo huo. 

Ligi ya Polisi Jamii wilaya ya Nyamagana iliyobuniwa na Jeshi la Polisi Nyamagana kupitia polisi jamii na kubatizwa jina la Nyamagana Cup imehusisha mpira wa miguu na mpira wa pete na kushindanisha timu 12 kutoka kata zote za wilaya hiyo, ambapo katika siku ya jana Timu ya Isamilo Queens imenyakuwa ubingwa kwa kuitandika Mkolani Queen.

Mgeni rasmi  Noel Mtekateka akikagua kikosi cha washindi wa pili mpira wa pete kwenye mashindano ya Nyamagana Cup, Mkolani Queens.

Washindi wa pili Nyamagana Cup iliyomalizika jana Mkolani Queen katika picha ya pamoja.

Pamba Queen mabingwa wa Netiboli (mpira wa pete) wakiwa katika picha ya pamoja.

Meza ya kutunza kumbukumbu za michezo ikiwajibika wakati wa fainali hizo zilizofanyika jana viwanja vya Nyamagana jijini Mwanza. Lengo la mashindano hayo ni kupunguza vitendo vya uhalifu, kuwaondosha vijana vijiweni na mitaani na kuwaweka vijana pamoja kubadilishana mawazo na kujifunza mambo ya msingi ili kupunguza vitendo vya uhalifu.

Mchezo wa fainali ukiendelea baina ya Mkolani Queens na Pamba Queens ambapo mwisho wa siku Pamba Queens iliibuka kuwa Machampioni wa netiboli Nyamagana.

Kwa mara ya kwanza mashindano hayo yamevunja rekodi kwa kutokuwa na mchezaji yoyote aliyezawadiwa kadi nyekundu hadi yakifikia tamati hii ikimaanisha kuwa suala la nidhamu limezingatiwa kwa hali ya juu na washiriki wa mchezo huo. Mpango mzima Washindi watakabidhiwa zawadi zao mwishoni mwa wiki katika viwanja vya Line Polisi Mabatini. Tuwe sote..

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.