ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, July 13, 2012

ZANTEL YAHIMARISHA MAWASILIANO YA MADIWANI MWANZA

Mkurugenzi wa jiji la Mwanza Wilson Kabwe akionyesha simu aliyokabidhiwa na Zantel aina ya Blackberry
Kampuni ya mawasiliano ya simu za mkononi ya ZANTEL leo imekabidhi simu za mkononi zipatazo 50 kwaajili ya kuimarisha mawasiliano ya madiwani wa jiji la Mwanza ambapo wataweza kuongea bure baina yao wakati wote.
Diwani wa kata ya Mkolani Stanslaus Mabula akipokea simu toka kwa Mkurugenzi wa Masoko Zantel Deepak Gupta, anaye fuata ni Afisa masoko wa kampuni hiyo Sajid Khan na Mkurugenzi wa jiji la Mwanza W. Kabwe.
Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo Afisa biashara mkuu wa Zantel Bw. Sajid Khan alisema kampuni ya Zantel imekuwa mstari wa mbele kushirikiana na taasisi zinazowahudumia wananchi katika kuharakisha maendeleo katika maeneo mbalimbali.
"Huu ni mwanzo tu, Zantel ni kampuni ambayo inamilikiwa na Watanzania na tunaahidi kuendelea kushirikiana na taasisi pamoja na sekta binafsi ambazo zinawagusa wananchi moja kwa moja ili kuhakikisha maisha ya watanzania yanaimarika" alisema Bw. Khan
Msaada huo unatarajiwa kuwaunganisha na kurahisisha mawasiliano viongozi wa jiji hilo na pia utaondoa gharama zmbazo zingetumika kwa mawasiliano na kutumiaka kwa shughuli nyingineza kimaendeleo.
Uwezeshaji huo ni mwendelezo wa shughuli za kijamii za ZANTEL ambao wakekuwa wakiziwezesha halmashauri na manispaa za miji mbalimbali kwa sasa hapa nchini kimawasiliano.
Diwani wa kata ya Nyamagana Bhiku Kotecha akipokea simu toka kwa Mkurugenzi wa Masoko Zantel Deepak Gupta, anaye fuata ni Afisa masoko wa kampuni hiyo Sajid Khan na Mkurugenzi wa jiji la Mwanza W. Kabwe.






Akizungumzia msaada huo Mkurugenzi wa jiji la Mwanza, Wilson Kabwe ameishukuru kampuni ya zantel na kupongeza juhudi zake ambazo zlisema jiji hilo linazihitaji sana hasa kipindi hiki ambapo jiji linazidi kukua kwa kasi likihitaji mawasiliano rahisi kufikisha utoaji taarifa.

"Tunaahidi kuwa uwezeshaji huu utasaidia wananchi moja kwa moja hasa ukizingatia kuwa madiwani ni kiungo muhimu kati ya wananchi wa chini kabisa na Serikali" alisisitiza Bw. Kabwe.

Tupe maoni yako

1 comments:

  1. Hongera kwa kazi nzuri ya kutupatia habari motomto mr sengo ila mm nina pendekezo tu napenda tuboreshe blog yako na iwe na muonekana mzuri zaidi ya hapa kwani wewe ni mtu maarafu sana,
    usisite tuwasiliane kupitia my blog

    www.ramsoict.blogspot.com
    Mwanza-Tanzania

    ReplyDelete

Note: Only a member of this blog may post a comment.