ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, July 10, 2012

WATEJA MWANZA KUJISHINDIA FEDHA TASLIMU HADI Tsh 1M KWENYE VUTA MKWANJA NA Coca-Cola

 Kampuni ya vinywaji baridi jamii ya Coca-cola ya Nyanza leo imezindua promosheni ambayo itawawezesha watumiaji wa vinywaji vyake kujishindia zawadi za fedha taslimu hadi Tsh milioni moja. Zawadi nyingine za fedha taslimu ni
100,000/=
10,000/=
 5,000/=
2,000/=
fulana na soda za bure.

 "Nidhahiri kwamba promosheni tunayoizindua hivi leo itasaidi kuboresha maisha ya Watanzania watakaobahatika kushinda zawadi za fedha taslimu hasa wale ambao watajishindia ile zawadi kubwa ya Tsh milioni moja ambapo zawadi hiyo pindi mtu akijishindia tunamsihi afike moja kwa moja kiwandani ambako ndipo itatolewa" Alisema Meneja wa Masoko wa Nyanza Bottling Co. Ltd Bw. Alfred Malando.

Meneja wa Masoko wa Nyanza Bottling Co. Ltd Bw. Alfred Malando, akizungumza na wandishi wa habari waliohudhuria uzinduzi huo uliofanyika leo kwenye ukumbi wa mikutano kiwandani eneo la Igoma jijini Mwanza ambapo alisema kuwa promosheni hiyo itadumu kwa muda wa wiki nane na inafahamika kama Vuta Mkwanja na Coca cola.

Soda zenye vizibo rangi ya dhahabu sokoni ndizo zitakazo husishwa na shindano kapambe la Coca cola linalojulikana kwa jina la Vuta Mkwanja na Coca cola linaloambatana na kaulimbiu iliyonasa vinywa vya wengi 'Sababu bilioni moja za kuthamini Afrika'.

 Zawadi ya soda ya BURE, Tsh 2,000, hadi 10,000 zitatolewa papo papo na wauzaji, vituo vya mauzo ya jumla na wauzaji wa jumla na wauzaji wa jumla. zawadi ya LAKI MOJA itatolewa kwenye vituo vya maozo ya jumla na wauzaji wa jumla huku washindi wa MILIONI MOJA watakabidhiwa zawadi zao kiwandani (Nyanza Botling Company Limited) 

 Sehemu ya wandishi wa habari walioalikwa kuhudhuria uzinduzi huo wa promosheni ya Vuta Mkwanja na Coca cola hii leo.

Wadau wa kampuni ya kutengeneza vinywaji baridi jamii ya Coca cola jijini Mwanza (Nyanza Botling Company Limited) wakitambulisha moja kati ya soda zitazo wanufaisha wananchi pindi watakaponunua vinywaji hivyo na kuangalia chini ya kizibo kukutana na zawadi kemkem za kujishindia.

Tupe maoni yako

1 comments:

Note: Only a member of this blog may post a comment.