TSC Sports Academy wakisali (mikononi wakiwa na vitambaa vyeusi) kuwakumbuka ndugu wote waliopoteza maisha kwenye ajali ya meli iliyotokea Zanzibar.. |
TSC Academy (white) 2 vs 1860 Munich (black) 2 katika uwanja wa Mannheimer Wasserturm. |
Timu U20 ya TSC Sports Academy, imeanza mashindano ya Inselcup, katika kundi B kwa kutoka sare ya magoli 2 kwa 2 na timu ngumu kabisa ya 1860 Munich, ambayo ni moja ya timu bora 5 katika ligi ya vijana ya Ujerumani. Magoli ya TSC ya lifungwa na Saidi Hassan katika kipindi cha kwanza, na Tito Jonathani aliongeza bao la kuongoza katika kipindi cha pili.
Sehemu ya mashabiki waliohudhuria mchezo huo. |
Mpango mzima wa makundi, TSC Mwanza wawakilishi wa Tanzania wakiwa kundi B |
Katika mechi nyingine za kundi A zilizofanyika katika uwanja huo huo wa Mannheim (Uliopo jimbo la Mannheim) hapa Ujerumani, Timu wenyeji -SV Waldhof Mannheim 07 walifungwa na H.N.K Hajduk Split ya Croation Magoli 2 - 0
Pia katika kundi hilo timu ya........SPVGG 03 Ilvesheim iko katika daraja la chini kabisa ligi ya vijana Ureumani, walifungwa goli 7-0 na timu ya Karlsruher Sports Club ambayo ipo kwenye moja ya nafasi za juu katika ligi ya vijana Ujerumani.
Nembo ya Urafiki baina ya Ujerumani na Tanzania kupitia salamu yetu iliyobuniwa na vijana wetu wenye vipaji vya soka. |
Timu ilipowasili eneo la michezo wakiongozwa na Mkurugenzi wa TSC Mutani Yangwe aka 'bwana harusi' (mbele mwenye nguo tofauti). |
TSC wanadhaminiwa na kampuni ya vifaa vya michezo ya ADIDAS ya nchini Ujerumani ambapo kampuni hiyo imetoa nyenzo zote kwa michezo na matembezi kwa wachezaji wa timu hiyo. |
TSC jukwaani na picha ya pamoja. |
Mazoezi ya vijana wa TSC wenye umri wa chini ya miaka 20 |
Mazoezi yakiendelea. |
Nyanda wetu. |
Majembe yetu Kabai na Miraji |
Matokeo zaidi kwa michezo mingine na safari ya TSC kwa ujumla utayapata hapa hapa pia waweza kufuatilia matokeo mengine na chakato wa ligi nzima kupitia (www.inselcup.com) |
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.