ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, July 9, 2012

"TRENI YA ABIRIA MWANZA KUANZA KUFANYA KAZI SEPTEMBA" YASEMA SERIKALI


Serikali Imesema treni ya abiria kati ya Dar es salaam na Mwanza, itaanza safari zake mwezi Septemba mwaka huu baada ya kufufua vichwa treni hiyo .
 Kauli hiyo ilitolewa leo na Naibu Waziri wa Uchukuzi, Dkt Charles Tizeba, wakati akizungumza na watumishi wa Mamlaka ya Bandari (TPA), Kampuni ya Huduma za Meli (MSCL) na Kampuni ya Reli (TRL) Alisema serikali itafanya kila liwezekano kuhakikisha treni hiyo inaanza safari zake ili kuwezesha wanchi kutumia treni hiyo kusafirisha mizigo na biria kama ilivyokuwa zamani.
Alisema kuwa uhalifu wa Watanzania ulichangia kuiuawa reli ya kati itokayo Dar es saalam hadi Mwanza, ambapo TRL inakusudia kununua injini mpya 13, kukodisha vingine 18 kutoka nchini Afrika Kusini na itafufua vingine 15 ili kuiwezsha treni hiyo kufanya kazi mwaka huu . “Kabla ya Septemba katika mwaka huu wa fedha treni ya abiria kuja Mwanza itaanza kufanya kazi.Sijawahi kushindwa, tutasukumana na kununiana lakini lazima treni itembee, na hiyo ndiyo ahadi yangu kwenu,” alisema Dkt Tizeba.
Alisema kuwa baadhi ya watumishi walichangia kuiawa TRC kwa kuiba vipuri, kuharibu miundo mbinu ya reli, kwani watumishi hao ndiyo wanaofahamu thamani ya miundo mbinu na vifaa vya reli na wanahafamu lilipo soko la vitu hivyo. Kwamba udokozi wao ulisababisha shirika hilo kujiendesha kwa hasara. ‘Wezi wasipate nafasi, nafahamu upo wizi wa mafuta, nakuomba meneja usafiri nao ili kubaini kiasi cha mafuta kinachotumika kuja Mwanza na kurudi Dar es salaam, vinginevyo watakupiga hasara kila wakirudi. Mazungumzo ya mwizi yawe mlango wa kutokea ule pale,” alisema na kuongeza
“Watumishi hawajali kutunza mali za kampuni,lakini TRL mambo yenu ni lawama zote kutupwa RITES , yapo mambo hayakuletwa na RITES yalikuwepo tangu wakati yupo Mboma, tuwe makini na tusiwalaumu Wahindi mambo yalishaseleleshwa na waswahili .”
Alionya watumishi wa kampuni hiyo kutoingia mkenge wa kushirikiana na watu, hasa wafanyabiashara ya usafirishaji wa mizigo kuhujumu reli, kwani baadhi wapo wanahusika na wanatumika kuhujumu miundo mbinu ya reli yetu.
Naibu waziri huyo aliutaka uongozi na manejimenti ya TRL kuwatumia watalaamu waliopo kuonyesha ujuzi wao katika kutengeneza motor za vichwa vya treni, ili kuokoa fedha zinazolipwa kwa wageni vinakopelekwa utengenezwa.
Aidha alishauri uongozi kuingia mikataba ya usafirishaji mizigo ili kuwezesha kampuni kupata mikopo itakayosaidia kuboresha na kutatua changamoto zinazoikabili kampuni hiyo, ambapo alisema watumishi wake wameongezwa mshahara na kuwataka wajitume bila hivyo mishahara haitaboreshwa bila reli kufanya kazi . Alidai kuwa serikali haiwezi kufufua reli kwa kutegemea fedha za bajeti, vingine ikope ili kujenga reli ya kisasa .
Alionya watumishi wanaouza tiketi za abiria kinyume na nauli iliyopangwa, wakibainika sheria itachukua mkondo wake, ambapo aliwaonya watumishi wa TRL walipo kwenye mzani wa Tabora kuacha kuibia kampuni na kujitajirisha.
Awali Kaimu Mkurugenzi wa TRL Kisamfu Kipallo, alimweleza Naibu waziri kuwa kampuni hiyo inakabiliwa na uhaba wa vitendea kazi,kwamba kuimarika na kuanza kutumia kwa reli hiyo kutachangia kukuza uchumi wa taifa.
“Uchakavu wa mabehewa na vipuri,watumishi ni wachache. Reli hii ikiimarika tutaweza kusafirisha mizigo kwa gharama nafuu na kuziacha barabara zetu zidumu kwa miaka mingi. Zamani tulikuwa na treni 3 za abira baada ya ubinafsishaji zikafia 4 lakini leo hakuna hivyo kurejeshwa kwake ni faraja kwa wananchi, ”alisema Kimsafu.
Alisema katika kipindi cha mwaka jana waliweza kusafirisha mizigo ya tani (1/2) nusu milioni kulinganisha na tani za mizigo 1.4 milioni mwaka 2002.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.