ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, July 25, 2012

ISAAC SHINYELA AZUNGUMZIA LOGO MPYA YA MANISPAA YA ILEMELA

Logo mpya iliyopendekezwa ambayo bado haijapitishwa.

Nimeipenda idea ya Ilemela kujitegemea kama manispaa huru. Sifahamu vizuri kuhusu muundo mpya wa utawala wa jiji utakavokua pindi Ilemela itapokua manispaa. Lakini nadhani muundo bora ni ule kama wa jiji la Dar es Salaam, yani pawe na Nyamagana Municipal Council, Ilemela Municipal Council na Mwanza city council. Mwanza city council iwe kama muhimili mkuu wa jiji na iwe na mayor wake (meya wa jiji kama alivyo Masaburi Dar es Salaam) halafu kila council (Ilemela na nyamagana) iwe na meya wake pia.
Naomba kuwasilisha Pendekezo la logo aliyoidizaini mdau Shinyela.


Muundo kamili unakuwa na mameya watatu wanaokalia ofisi tatu tofauti. Mapendekezo yaliyopo ya kuwa na Mwanza city council na Ilemela Municipal council yanapaswa kutazamwa upya kwani tunapo ongelea Mwanza city, tunamaanisha Nyamagana na Ilemela. Hivo basi kama tunaamua kutawanya majukumu ya city council, basi zizaliwe manispaa mbili; Nyamagana na Ilemela halafu city council iwajibike katika ngazi ya juu ya manispaa hizi mbili.


Kitu kingine ni pendekezo la nembo ama logo ya mnispaa ya Ilemela, mi nadhani haijakaa vizuri na haivutii. Imekaa kizamani sana. Kama ningalikua mimi ndie msanifu wa logo hiyo, ningesanifu logo inayokwenda na wakati na si kisamaki kimening’inia. Binafsi ningesanifu logo hiyo hivi:

Shinyela, Isaac
July 2012

Tupe maoni yako

1 comments:

Note: Only a member of this blog may post a comment.