KAMATI ya
Siasa ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Mwanza imetengua na kumvua nafasi
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi Benald Pollycarp baada ya
kukaidi maagizo na maelekezo ya yaliyotolewa na kamati hiyo kwa Kamati ya siasa
ya Wilaya ya Misungwi hivi karibuni.
Akitoa Tamko la Kamati hiyo ya mkoa iliyoketi kwenye ofisi za mkoa leo jioni na kufikia uamuzi huo Katibu wa siasa na Uenezi wa CCM mkoa Saimon Mangelepa amesema kwamba kutokana na maagizo iliyokuwa imeyatoa kwa kamati ya siasa ya wilaya ya Misungwi ambapo pia ilimwita na kumhoji mwenyekiti huyo kisha kumtaka apime uzito wa tuhuma na kujiuzuru nafasi hiyo.
Pollycarp anatuhumiwa kuhusishwa na ubadhilifu
na wizi wa fedha za halmashauri ya wilaya ya Misungwi kwenye taarifa ya Mkaguzi
mkuu na Hesabu CAG Ludovick Uttouh iliyozitaja Halmashauri 33 nchini ambazo
zimeripotiwa kutafuna fedha kinyume cha taratibu na kanuni za kwa malengo
yaliyokuwa yamekusudiwa ikiwa ni utekelezaji wa miradi ya
maendeleo.
Wakati
uongozi wa CCM ngazi Mkoa wa Mwanza ukichukua hatua na maamuzi hayo tayari kumekuwepo
na tetesi kuwa mwenyekiti huyo amekuwa akiendesha mikakati ya chini kwa chini
kuwahamasisha baadhi ya madiwani wenzake 26 wanaomuunga mkono waendelee
kujiandaa na kukihama chama hicho na kujiunga na chama kimoja cha siasa kwa
madai kwamba taarifa hiyo ya CAG iligushiwa na kuchakachuliwa kwa lengo la
kisiasa ikidaiwa kufanywa na kigogo mmoja wa ngazi ya kitaifa atokaye Wilayani
humo.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.