Jaji Mstaafu J. Warioba. |
Wajumbe Zanzibar. |
Katika mkutano wa leo na ule uliofanyika jana (Jumanne, Juni 19, 2012) jijini Dar es Salaam, Jaji Warioba amesisitiza umuhimu wa vyombo wa habari kushiriki kikamilifu katika kuwaelimisha wananchi kuhusu mchakato wa kupata Katiba mpya unaoendelea na kuahidi kuvipa ushirikiano vyombo vya habari.
Wajumbe. |
Jaji Warioba aliongeza kuwa wananchi hao wanasema kuwa mamlaka ya taasisi za dola kama vile Serikali, Bunge, Mahakama, Tume mbali mbali za kikatiba, na hata Vyama vya Siasa, yamefafanuliwa, hali ambayo ni tofauti na mamlaka ya wananchi.
Wajumbe mkutanoni. |
Aliyataja maeneo hayo kuwa ni kuheshimu na kuthamini utu na haki nyinginezo zote za binadamu; utekelezaji wa shughuli za Serikali kwa njia ambazo zitahakikisha kwamba utajiri wa Taifa unaendelezwa, unahifadhiwa na unatumiwa kwa manufaa ya wananchi wote kwa jumla na pia kuzuia mtu kumnyonya mtu mwingine.
Sehemu ya kutano hilo. |
Wakitoa maoni yao katika mkutano huo, waandishi wa habari, pamoja na kupongeza uamuzi wa Tume kukutana nao, walishauri wananchi wahakikishiwe uhuru wa kutoa maoni ili kuwawezesha kushiriki kikamilifu bila woga.
"Baada ya kukusikiliza, ninaona utashi wa Tume kufanya kazi kwa uwazi na uhuru. Lakini kwa hali inavyoendelea hususan hapa Zanzibar, nadhani inabidi wananchi wahakikishiwe uhuru wa kutoa maoni," alipendekeza Jabir Idrissa, Mhariri wa gazeti la Mwanahalisi aliyepo Zanzibar.
Mkutano wa leo ni wa pili na umewalenga waandishi wa habari waliopo Zanzibar. Kesho Jaji Warioba ataongea na Wakuu wa Wilaya na Mikoa kutoka Zanzibar. Tume tayari imeshafanya mikutano na Wakuu wa Mikoa na Wilaya wa Tanzania Bara katika semina iliyofanyika mjini Dodoma mwezi uliopita.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.