ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, June 11, 2012

SERENGETI YAENDELEZA KAMPENI KUDUMISHA MILA NCHINI KWA KUDHAMINI MSIMU WA MAVUNO BULABO

Mgeni rasmi mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mwanza Clement Mabina akifungua rasmi mashindano ya ngoma za msimu wa mavuno kwa kabila la wasukuma (Bulabo)  katika viwanja vya Red Cross kijiji cha Kisesa  wilayani Magu mkoani Mwanza.
Mkurugenzi wa Idara ya Masoko ya SBL, Ephraem Mafuru akishiriki kuzindua mashindano hayo yanayoshindanisha vikundi vya ngoma Wagika na Wagaru vya kabila hilo, katika kuadhimisha na kusherehekea mavuno kila mwaka, ambapo  vikundi 30 kutoka maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Mwanza zimethibitisha kushiriki.
Kundi hili la Makirikiri ya Shinyanga lilicheza ngoma kwa mvuto na style ya kipeke hivyo kuvutia wengi.
Hapa ngoma imepambamoto kwa picha za mavideo zaidi tegeshea jicho lako Clouds Tv.
Clouds Tv ilikuwepo tukioni kuchukua kila hatua za mvuto kwa msimu wa mavuno (Bulabo)
Si katika bongo fleva pekee hadi ngoma asili kuna wasafi aka 'masharobaro'
Ngoma za Bulabo zilianza mnamo mwaka 1700 kabla ya kuboreshwa na kuingizwa katika Kanisa Katoliki mwaka 1954, ambapo ngoma hizo za asili zilichezwa na kushindanisha makabila ya Wagika na Wagalu
Kikundi kingine.

Chekshia engo adimu.

Ili watoto waone yanayojiri...

Ngoma tamu.

Watu wamejipanga bwana.

Ngoma za utamaduni za asili ya kabila la Wasukuma ‘Bulabo’, zimepata udhamini wa sh. milioni 12 kutoka Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) kupitia bia ya Serengeti.
Akizungumza na waandishi wa habari, Mkurugenzi wa Idara ya Masoko ya SBL, Ephraem Mafuru alisema udhamini huo ni kwa ajili ya kuwezesha washiriki wa tamasha hilo la ngoma za asili za Bulabo mwaka huu
Mdau wa Kambi popote Antonio Nugaz pia alikuwepo kuchukua Clip za tukio hamu yake ni kuona Fisi anavyoshirikishwa kwenye ngoma za watu wa kabila la Kisukuma kisha kukumegea mdau ndani ya Kambi Popote na Clouds TV.
Ili kunasa matukio kwa utamu....
Tunasubiri zamu yetu... wadau wa vikundi vya ngoma.
Ngoma hizi zitadumu viwanjani hapa kwa muda wa siku 8 ambapo jumapili ndiyo siku ya fainali, mshindi atatangazwa na wananchi watachinja ng'ombe na wote kula katika viwanja hivi. Hasa ukizingatia kuwa Mh. Rais wa Jamhuriya Muungano wa Tanzania Jakaya Kikwete keshatoa ng'ombe 14 kwa ajili ya kunogesha sherehe "...hii wajameni ...sikosi" 
Nyomi.
Hongera kwa watu wa kabila la Sukuma.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.