Madiwani wakipitia kablasha la bajeti kwenye kikao cha Baraza hilo kilichofanyika mwishoni mwa wiki.
Wenyeviti wa kamati za kudumu za Baraza la Madiwani kulia John Minja mwenyekiti wa kamati ya huduma za jamii, afya na elimu na kushoto ni mwenyekiti wa kamati ya Mipango miji Henry Matata.
Moja ya hoja binafsi iliyoungwa mkono na madiwani wote kwenye Baraza hilo ni kwamba kila kata ianze kuwatumia vijana wasio na ajira kuzibua mitaro kwa vifaa maalum na kulipwa na halmashauri hiyo kwa lengo la kukabiliana na changamoto ya ajira nchini, hoja iliyowasilishwa na diwani wa kata ya Nyamagana Bhiku Kotecha.
Diwani wa kata ya Igoma Adam Chagulani akichangia hoja ya rasimu ya bajeti ya jiji la Mwanza.
Baraza likiendelea huku walioketi juu ni wananchi wakifuatilia kikao hicho.
Mweka hazina wa Halmashauri ya jiji la Mwanza Wiliam Ntinika akiwa na wataalamu wenzake wakifuatilia na kuchukuwa hoja za baadhi ya madiwani ili kuzitolea ufafanuzi kwenye baraza hilo.
Hivi ndivyo huketi wakati wa kikao cha baraza la Madiwani wa Halmashauri ya jiji la Mwanza.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.