ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, May 7, 2012

WAKUFUNZI TOKA CLUB YA ARSENAL YA UINGEREZA WAANZA KUPIGA MSASA MAKOCHA WA MWANZA

Mafunzo ya wiki moja kwa makocha wa mpira wa miguu kwa vituo mbalimbali yameanza leo jijini Mwanza yakishirikisha zaidi ya makocha 40 wa shule za msingi, za sekondari na timu za vijana wa mitaani.

Mmoja kati ya makocha wawili waliotua jijini Mwanza, Alikhan Popat kutoka katika mradi wa kukuza mpira wa jamii club ya Arsenal ya Uingereza akieleza sababu zao kuwa nchini na mchakato mzima wa mafunzo hayo...

John Olaleye (raia wa Msumbiji aishiye nchi Uingereza) akiwa naye ni mkufunzi kutoka mradi wa kukuza mpira wa jamii club ya Arsenal ya Uingereza amesema kuwa makocha wa timu ndogondogo jijini Mwanza watapata fursa ya kujifunza mbinu mbalimbali ambazo ni msingi muhimu kulea na kukuza vipaji hali itakayo warahisishia makocha wa timu za madaraja ya juu na Taifa kwa ujumla.
Kwamujibu wa Mkurugenzi wa kituo cha soka cha Tanzania Sports Academy (TSC) Mutani Yangwe amesema kuwa mafunzo hayo yanaratibiwa kwa ukaribu na Club ya Arsenal ya nchini Uingereza na wenyeji TSC yamekuja yakiwa na lengo kuu la kuimarisha na kuwajengea uwezo Walimu wa timu za soka kwa shule za msingi, sekondari na timu mbalimbali mitaani.
Wakufunzi John Olaleye na Alikhan Popat wakijumuika na makocha wa Mwanza kufundisha moja kati ya mbinu muhimu za awali kwenye mazoezi ya kunyoosha viungo ambapo kwa upande wao wamesisitiza kuwa kocha mzuri ni yule anayefundisha kwa vitendo.

Makocha wazawa wakijumuika mafunzoni...

Mafunzo yakiendelea kwa makocha wetu...

Hakika soka inatumia lugha moja duniani kote..

Licha ya kubainisha kuwa mafunzo hayo ni sehemu ya kubadilishana ujuzi mkufunzi mwandamizi wa soka nchini kutoka kituo cha TSC, Rogashian Kaijage amebainisha kuwa mchakato huo wa mafunzo utasidia kuwarahisishia hata makocha wa vilabu ngazi za juu kupokea vipaji vilivyoshiba misingi ya soka na si kupokea wachezaji mbumbumbu wa misingi ya soka kama ilivyo kwa vilabu vingi nchini hali inayopelekea taifa kufukuza makocha kila kukicha, zaidi sikiliza SPORTS EXTRA ya CLOUDS FM leo.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.