ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, May 22, 2012

UMESHAWAHI KUJIULIZA KWANINI WATU WENYE ALBINISM WANATIZAMA KIUPANDE UPANDE?

Umeshawahi kujiuliza juu ya watu wenye ulemavu wa ngozi na uono hafifu (Albinism) kwanini wanatizama kiupandeupande kwa kutumia jicho moja au kusoma kwa kufumbafumba macho au wakitembea kwa kuinamisha kichwa kama wanachungulia vile au pengine kusoma kwa kusogelea maandishi?

Wengi tukiwaona katika hali hiyo tunawaona kama watu wasiokuwa na akili sawa (wenye taahira ya akili) lakini kuna sababu juu ya hilo... Kutana na Professor Rebecca Kammer kutoka Southen California College of Optometry (katika video hapo juu) wakati akizungumza na walimu waandishi wa habari jijini Mwanza nchini Tanzania.

Tayari watoto zaidi ya 300 nchini Tanzania wamenufaika na mpango wa ugawiwaji miwani, vidarubini vidogo kwaajili ya kusomea, kofia maalum za kujikinga jua pamoja na ufadhili wa elimu kwa watoto hao, Professor huyo bado yuko nchini kwa ajili ya kuendeleza zoezi la upimaji na uchunguzi wa macho kwa watoto wenye ulemavu wa ngozi ambao wengi wanauoni hafifu chini ya mpango unaoratibiwa na Shirika la Under The Same Sun.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.