ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, May 8, 2012

TZ ZAIDI YA UIJUAVYO NDANI YA KAMACHUMU

Wakati Tanzania ikiwa katika miaka 50 ya Uhuru sasa, Mnara huu ulijengwa katika maadhimisho ya miaka 10 ya Uhuru, mnara uko kwenye kipita shoto cha njia panda ya wilaya ya Muleba mkoani Kagera kuelekea Nshamba, Ndolage Hospital, Lutabo na Bukoba mjini, "Ukarabati basi ufanyike kulinda kumbukumbu...!".
Wakazi wa mkoa wa Kagera, ndizi ni moja kati ya mazao makuu ya biashara, style ya uhifadhi, upakiaji na utunzaji ni ya kipekee kabisa tofauti na mikoa mingine nchini kama ulaya vile kwamba ndizi bora nizile zisizokuwa na makovu yanayopenya hadi ndani na zao hili sokoni wao huliweka kwenye madaraja.

Baada ya zao la kahawa kudorora mkoani humu hivi sasa zao hili limeshika biashara ingawa kuna changamoto ya ugonjwa wa mnyauko unaonyemelea, hapa ni soko la kila siku la ndizi linalopatikana Kamachumu Centre.

Tizama upakiaji kupitia usafiri wa baiskeli toka vijiji vya mbali hadi sokoni hapa yaaani 'smati'.

Magimbi fungu Tsh 200/= tu! Kweli kwetu pazuriiii....

Msimu wa senene unapowadia vijana wengi wasio na ajira hujipatia kipato kwa kazi ya kutoa mabawa ya senene kwa mapatano kuanzia Tsh 20,000/= na kuendelea kwa gunia.

Wananchi wengi wamekuwa wakinufaika sana hata wengine kujenga majumba, kusomesha watoto na kuendesha maisha kupitia biashara hii ya senene ambayo imekuwa maarufu si nchini tu kwa kitoweo bali hata nchi za mbali.

Bodaboda ajira nyingine kituo cha mabasi Kamachumu.
 PICHA ZOTE NA MDAU WA G.Sengo Blog Samadu Abdul

Tupe maoni yako

2 comments:

Note: Only a member of this blog may post a comment.