Ongezeko la tafiti katika eneo la mazoezi na magonjwa yahusianayo na mifumo ya maisha (lifestyle-related diseases) limeongezeka katika miaka ya sasa hatimaye majibu yakaweza kuwafumbua macho wengi juu ya umuhimu wa mazoezi katika kujikinga na kutibu magonjwa mbalimbali.Tafiti katika eneo hili zinaonesha kwamba mazoezi yanaweza kutumika kujikinga na magonjwa zaidi ya ishirini na kutibu magonjwa takribani kumi.Ni jambo lililowazi kabisa kwamba babu zetu waliweza kuishi kwa miaka mingi zaidi ya kizazi tulichopo sisi. Ni dhahiri pia kwamba kizazi chetu kinashuhudia milipuko ya magonjwa ambayo babu zetu hawakuwahi hata kuyasikia. Pia mtakubaliana nami kuwa, kumekuwa na mambo mengi ya kimaendeleo yaliyotokea katika kipindi chote hiki, ambayo wanazuoni wamekuwa wakiyahusisha na milipuko ya baadhi ya magonjwa. Yapo mambo mengi katika mifumo yetu ya maisha ya kila siku yaliyo mazuri katika muonekano na hisia, lakini ukweli ni kwamba yaweza kuwa na athari kubwa kwa afya zetu.watu kula zaidi na kutembea kidogo, kwa maana ya kuendesha magari na kuketi kutizama runinga kwa muda mrefu hii inaufanya mwili kutunza virutubisho ambavyo kwa hali ya kawaida vingetumika kama mtu angetembea au kufanya kazi itumiayo nguvu kiasi. Mwili hauhitaji kiasi kikubwa cha virutubisho hivi na baada ya muda mrefu vinakuwa kama sumu na hivyo kusababisha magonjwa kama vile kisukari kisichotegemea insulini (Type 2 diabetes).Kwa kufanya mazoezi, mtu anauwezesha mwili wake kutumia virutubisho ipasavyo, kwa maana ya kwamba hakuna kinachohifadhiwa mwilini kinyume na matakwa ya mwili.
Karibu sana Family Fitness Centre Ghana Mwanza.
Says Hassan Herry aka 'Kidume' aka 'Panadol'
Karibu sana Family Fitness Centre Ghana Mwanza.
Says Hassan Herry aka 'Kidume' aka 'Panadol'
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.