ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Sunday, December 25, 2011

RAIS KULIMBIKIZIWA MADARAKA BADO KIKWAZO KUELEKEA UUNDWAJI WA KATIBA MPYA NCHINI

Jana katika ukumbi wa Victoria Anex Furahisha mkoani Mwanza kulifanyika mdahalo wa kujadili uundwaji wa katiba mpya ulioendeshwa na Muungano wa Taasisi zisizo za kiserikali mkoani Mwanza (MNGONI) Katika mdahalo huo uliofanyika jana mkoani Mwanza wananchi wameomba kuondolewa kwa kifungu cha sheria kinachompa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, madaraka makubwa ya kuteua viongozi katika ngazi za juu serikalini.

Mr. Khassian
Wandishi wa habari tuandike habari zetu tukilenga kuwafundisha wananchi na siyo kuwapotosha kwani elimu ya Katiba pya inahitaji ushiriki mkubwa sana wa wandishi wa habari.

James Robare - Vice chairman TANVU.
Watanzania wapewe muda wa kutosha kuchingia mapungufu ya katiba.

Elimu tosha bado haijafika kwa wananchi ili marekebisho yawe sambamba na matakwa ya wananchi husika.

Aidha, baadhi ya wananchi walishauri rais asiruhusiwe kuteua Tume ya Uchaguzi ambayo imekuwa ikifanya kazi kwa matakwa ya rais mwenyewe bila kuwa huru, hivyo kushauri uteuzi huo kushirikisha wabunge wote ili haki iweze kutendeka.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.