Gary Speed aliwahi kuichezea Wales na kuwa nahodha wa timu ya taifa
Wanasema hakuna utata kuhusiana na kifo hicho, na inaelekea alijitoa roho.
Waziri mmoja wa Wales, Carwyn Jones, amesema hizo ni habari za kuhuzunisha na kusikitisha mno. "Ulimwengu umempoteza Gary Speed, mtu mashuhuri sana, na ninasikitika sana kwa kuwa ni jana asubuhi tu nilizungumza naye. Kwa nini? Kwa nini? Kwa nini? Nitamkosa sana maishani!", aliandika mchezaji mwenzake wa zamani, Robbie Savage, katika mtandao wa kijamii wa Twitter.
"Kimawazo tuko pamoja na familia yake wakati huu wa maombolezi."
Chama cha soka cha Wales FAW kilitangaza; "Tunatoa rambirambi zetu kwa familia yake".
"Tunawaomba wote kuhiheshimu familia yake na kuwaachia fursa ya kuomboleza wakati huu wa huzuni mno." Speed, ambaye alipata tuzo ya MBE mwaka 2010 kutokana na jitihada zake katika soka, Gary Speed alikuwa na umri wa miaka 42 amemwacha mjane na watoto wawili.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.