Katika Mkutano huo mambo makuu manne yalijadiliwa kwa kirefu na kutolewa muafaka likiwepo suala la Soko la Fresh beans kushuka bei ambapo Ilidhihirika wazi kuwa Wanunuzi wakubwa wa zao hilo kwa sasa ni kutoka Kenya nayo makampuni kutoka nchini humo yakiongezeka siku baada ya siku.
Mbinu inayotumiwa na Wanunuzi hawa ni kununua kwa bei tofauti tofauti kutoka kwa Mkulima Mmoja hadi mwingine bila kuwa na Mkataba wa aina yoyote kitu ambacho kimepelekea Wakulima hao kuuza mazao yao kwa bei ya Chini. Pili wakulima hao waliazimia kuunda chombo cha Wakulima kusimamia ushawishi wa bei nzuri na kuwa wakulima wote watauza kwa kuzingatia bei iliyopitishwa.
Aidha ili kufanikisha utekelezaji wa shughuli za wakulima na kutoa mwelekeao sahihi katika bei na utetezi sahihi juu ya maslahi ya Wakulima kwa kuwa na sauti kuu ya pamoja wakulima kwa pamoja walipendekeza na kukubaliana kuunda Umoja wa Vikundi vya Wakulima (Commercial Farmers Associations_CFA) wa Fresh Beans kutoka Wilaya za Arusha DC na Meru DC.
Changamoto nyingine iliyojitokeza katika mkutano huo ilikuwa ni Mtaji kwenye kilimo hicho hasa pembejeo kama mbolea, mbegu na ukosefu wa mtaji ambao umewageuza wakulima hao kuwa vibarua kwa mashamba yao huku wenye pesa kumiminika kwa wingi kwenye mashamba yao kwa kutoa fedha na kuyakodisha mashamba hayo kujinufaisha wakiwaacha wakulima hao dhoofu in hali.
Kwa kauli moja Wajumbe hao wamekubaliana na kuweka Mkakati wa kuanzisha Vikundi vya kuweka na Kukopa (VICOBA Village Community Bank) ambapo kila Mkulima atapaswa kuchangia kiwango fulani ili kumpa fursa ya kupata fedha pindi anapohitaji.
TAHA kwa upande wake ikiwakilishwa na Mr. Isaac Ndamanhyilu ambaye ni Afisa Utetezi Jamii wa TAHA, amesisitiza juu ya Wakulima hao kuwa na Umoja ili kujenga sauti ya pamoja na kuwa TAHA ipo sambamba nao katika kufanikisha yote waliyokubaliana kwani ni jukumu lake kufanya hivyo.
Kikao Kingine Kitafanyika Tarehe 8/10/2011
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.