ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Sunday, July 10, 2011

KAGERA YAIBUKA KIDEDEA YATWAA UBINGWA WA MASHINDANO YA NGOMA YA BALIMI EXTRA LAGER

Kiongozi wa kundi la Rugowoire kutoka mkoani Kagera akichekelea kitita cha Tsh. 1,000,000/= baada ya kukabidhiwa na mgeni rasmi wa mashindano ya Ngoma ya Balimi Kanda ya ziwa, Kaimu mkurugenzi wa jiji la Mwanza Bw. Patric Karangwa.

Kundi la Kiwajaki kutoka Mkoani Mara, likitoa ujumbe wa Bia ya Balimi Extra Lager.

Kundi la Magombegakijiji kutoka Mwanza, likiingia tayari kuonyesha manjonjo yao ndani ya uwanja wa ccm Kirumba katika mashindano ya ngoma ya Balimi Extra Lager.

Kiongozi wa kundi la Mangombegakijiji akiwajibika kwa kupiliza pembe alisia ya nyati.

Kundi la Mwenge Taboro likitimbwilika na ngoma ya Mitete

Kundi la Egumba kutoka Mkoani Mara shughulini.

Fainali za Mashindano ya Ngoma ya Balimi Extra Lager, zimefanyika jana jumamosi katika uwanja wa CCM Kirumba zimemalizika kwa kundi la Rugowoire kutoka mkoani Kagera kutawazwa rasmi washindi na kujinyakulia kitita cha Tsh. 1,000,000/=

Katika mashindano hayo yalishirikisha jumla ya vikundi kumi kutoka mikoa ya Mwanza, Kagera, Shinyanga, Mara na Tabora, mshindi wa pili ni kundi la Utandawazi kutoka mkoani Mwanza ambao wameondoka na donge nono la Ths. 750,000/= Mshindi wa Tatu ni kundi la Mwenge kutoka mkoani Tabora ambao wameondoka na kitita cha Tahs. 500,000/=, Mshindi wa Nne ni kundi la Rugu kutoka mkoani Kagera ambao wamejinyakulia donge nono la Tsh. 400,000/= Mshindi wa Tano hadi wa Kumi wamejinyakulia kitita cha Tsh. 300,000/= kila kundi.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.