ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, June 27, 2011

SHULE ZA SEKONDARI MWANZA NA MAPAMBANO DHIDI YA MALARIA KWA NJIA YA SANAA

Imeelezwa kuwa asilimia 23 ya Watanzania ambao wanafaidika na msaada wa vyandarua vya kuzuia mbu wanaoambukiza ugonjwa wa malaria ndio pekee wanatumia vyandarua hivyo na wengine wameacha kuvitumia kutokana na imani potofu.Hayo yamesemwa leo na Meneja katika kitengo cha elimu katika Shirika la Mradi wa kuthibiti Malaria, Zinduka, Bi. Jojina Tesha wakati akiongea na wanafunzi kutoka shule mbali mbali za sekondari jijini Mwanza katika mkutano uliofanyika katika Shule ya Sekondari ya Pamba.

Amesema kuwa katika baadhi ya mikoa ambayo hadi sasa ametembelea kwa lengo la kuhasisha wananchi matumizi bora ya vyandarua ambavyo vimetolewa na serikali kupitia Wizara ya Afya tangu mwaka jana mwezi Augusti imeonyesha kuwa baadhi ya wananchi wamekuwa wakitumia vyandarua hivyo kwa matumizi mengine tofauti na malengo yaliyokusudiwa.


Mataluma..

Baadhi ya wananchi wamekuwa ni wagumu katika kutambua umuhimu wa kutumia vyandarua vilivyotiwa dawa kutokana na kuwa na zana potovu kuwa vyandarua hivyo vinasababisha kupunguza nguvu za kiume na wakati mwingine kusamabisha wanawake kutozaa, shirika la Zinduka limeamua kuwashirikisha wanafunzi wa shule za sekondari kutokana kuwa wao wana uelewa wa kutosha ili kuwaelimisha wazazi, walezi na watu wengine katika familia zao matumizi ya vyandarua na kwamba havina madhara yoyote kwa afya ya binadamu.

Kwa upande wake, Balozi wa Mradi wa kuthibiti malaria mkoa wa Mwanza, Bw. Farid Kubanda “Fid Q” amesema kuwa anatambua umuhimu wa wananchi kujikinga na ugonjwa wa malaria na kuongeza kuwa kwa kupitia sanaa, ataweza kupeleka ujumbe kwa wananchi unaolenga kutoa elimu juu ya kutokomeza ugonjwa wa malaria.

Masai wa THT na hisia zake akiimba mara baada ya kutoa meseji ya kujikinga na Maralia.

Kwa utulivu na usikivu....!!

Sam Wakweli

Bango.

Akiwa na yu mmoja wa mabalozi wa Malaria nchini Mwanadada Mwasiti nae alikuwepo kutia neno.

Sikubahatika kulinasa jina la kijana huyu anayesoma Pamba Sec ambaye alipata shavu la shangwe kupitia sesheni ya Zinduka free style, hapa alikuwa akipambana na Fid Q 'Ngosha the swagga Don'.

Sehemu ya wanafunzi toka shule mbalimbali za sekondari Mwanza waliohudhuria kusanyiko hilo.

Mtangazaji wa Clouds Fm Adam Mchomvu nae alipata fursa ya kuzungumza na wanafunzi kutoa elimu jinsi ya kujikinga na Malaria.

Wanafunzi wa Shule mbalimbali za sekondari walishiriki kuimba nyimbo zenye ujumbe wa kujikinga dhidi ya malaria ambapo shule zilizofanya vizuri zilizawadiwa.

Meza kuu.

Zawadi kwa washindi wa Zinduka Maralia free style.

Fid Q akisaini ma-Autograph.

Baba Joni na ma-Autograph.

Kampeni ya Malaria Haikubaliki, inaongozwa na serikali ya Tanzania chini ya Rais Jakaya Kikwete huku ikiungwa mkono na wahisani ambao ni pamoja na Malaria No More, Tanzania House of Talent, Chuo Kikuu Cha John Hopkins, Population Services International na United Against Malaria.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.