Mkutano huo wa nane wa wadau sekta ya kilimo cha Pamba umekuja na kauli mbiu isemayo 'Kilimo cha mkataba kitaleta mapinduzi kwa zao la pamba wadau tuthubutu'
Tayari wakulima wa Pamba wilaya ya Bariadi Mkoani Shinyanga wamejiunga na mfumo wa Kilimo cha Mkataba utakawawezesa kukopeshwa Pembejeo za kilimo na kuzilipa mara baada ya kuuza mazao yao.
Shamba la pamba mkoani Shinyanga.
Moja kati ya vijiji vilivyoanza kunufaika na mfumo huo ni kijiji cha Halawa, kilichopo katika kata ya Nkindwabiye wilayani humo ambacho wakulima wake wako katika hatua ya upaliliaji wa mimea ya zao la Pamba.
Hata hivyo katika mchakato mzima wa kufikia azma hiyo serikali imekumbana na changamoto zilizojitokeza siku za hivi karibuni kwani kumekuwepo na wimbi la udanganyifu katika ugawaji wa pembejeo za kilimo unaofanywa na baadhi ya watu wasiokuwa waaminifu kwa kushirikiana na wakala wa pembejeo pamoja na watendaji wa Kata na vijiji huku hali hiyo ikiacha wakulima wengi kukosa peembejeo ambapo waziri huyo ameahidi hulishughulikia suala hilo barabara.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.