ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, May 25, 2011

TEGETE AIPELEKA MWANZA FAINALI KILI TAIFA CUP

Timu ya mkoa wa Mwanza 'Mwanza Heroes' imekata tiketi kucheza fainali ya michuano ya Kombe la 'Taifa Kili Taifa Cup' baada ya kuifunga Ilala mabao 2-0 katika mchezo wa nusu fainali uliochezwa jana kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, mjini Arusha. Mwanza Heroes.
Mshambuliaji wa Yanga, Jerry Tegete alianza kuwainua mashabiki wa Mwanza kwa kufunga bao la kwanza dakika 45 baada ya kuwatoka mabeki wa Ilala kabla ya kufumua shuti kali lililojaa wavuni. Dakika 45 za kwanza, Mwanza ilicheza soka ya kiwango bora kwa kufanya mashambulizi mara kwa mara langoni mwa Ilala ambayo ilionyesha udhaifu sehemu ya kiungo na kutoa mwanya kwa wapinzani wao kucheza kwa nguvu.

Shangwe kwa ushindi kuingia fainali.
Kipindi cha pili kilianza kwa Mwanza kuliandama lango la Ilala na juhudi zao zilizaa matunda dakika 57 baada ya Tegete kufunga bao la pili kwa mkwaju wa penalti kufuatia mchezaji Erick Mawala kumfanyia madhambi Maregesi Mwangwa katika eneo la hatari akielekea kufunga.

Mwanza ilifuzu kucheza nusu fainali baada ya kuwafunga wenyeji Arusha mabao 2-1 katika mchezo wa robo fainali uliochezwa kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid. Nusu fainali ya pili itachezwa leo ambapo Mbeya 'Mapinduzi Stars' itavaana na Kagera.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.