ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, May 5, 2011

SAFARI YA MWISHO YA SOUND MAN WA ORIJINO KOMEDI ILIVYOKUWA

Mazishi ya Mtaalam wa sauti wa kundi maarufu la uchekeshaji nchini Mohamed Muya wa Orijino Komedi, aliyefariki hivi karibuni yamefanyika nyumbani kwao huko Korogwe mkoani Tanga na kuhudhuriwa na watu wengi wakiwemo ndugu jamaa na marafiki na wapenzi wa kipindi cha kundi hilo kinachorushwa TBC1.Wengi walihudhuria msiba huo kuhakiki habari zilizokuwa zimezagaa mtaani zikikanganya kwa wengi kupata habari kuwa mmoja wa wachekeshaji wa kundi hilo kaaga dunia huku wengine wakithubutu hata kutaja kwa majina.

Lakini kwa msada wa wahusika na TBC1 na redio kadhaa nchini walishiriki kutoa habari sahihi zikimtaja Sound man wa kundi hilo Mohamed Muya kuwa ndiye aliyefariki dunia.

Mwili wa marehemu uliwasili mjini Korogwe marafiki na wakazi wake kupata fursa ya kutoa salamu za rambirambi.

Akiwa na majonzi mazito mtoto wa marehemu Mohamed Muya aitwae Ommy (mdogo kuliko wote) akishuhudia safari ya mwisho ya baba yake.

Hapa ndipo alipolala ndugu yetu Mohamed Muya.
"Ewe Mola mpumzishe kwa amani kiumbe wako"
Amina.


HABARI ZAIDI TEMBELEA www.mkandamizaji.blogspot.com

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.