ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, May 7, 2011

MWANZA, SHINYANGA WAANZA VYEMA KILI TAIFA CUP KITUO CHA MWANZA.

Timu ya mkoa wa Mwanza.
Wenyeji wa michuano ya Kili Taifa Cup kituo cha Mwanza Herous leo wametumia vyema uwanja wao wa nyumbani baada ya kuibamiza timu ya mkoa wa Kagera Rweru Eagles 2-1 mchezo uliochezwa kwenye dimba la CCM Kirumba.

Mabao ya Mwanza Herous yalipatikana katika kipindi cha kwanza, goli likifungwa na Malegesi Mwangwa (36), dakika 3 baadae ikaandika bao la pili kupitia winga wake machachari Jerison Tegete aliyefunga kwa ufundi mara baada ya kuwapiga vyenga mabeki wa Kagera na hatimaye kuukwamisha mpira kimiani.mkuu wa mkoa wa mwanza Abass Kandoro akisalimiana nae Jerison Tegete kabla ya mchezo baina ya Mwanza Herous na timu ya mkoa wa Kagera.

Kipindi cha pili dakika ya 62 Kagera wakapata goli kupitia mpira wa penati iliyofungwa na Juma Nade. Hadi kipindi cha mwisho Mwanza Herous 2, Kagera 1.

Mchezo wa pili baina ya timu ya Shinyanga wana Igembesabo na timu ya mkoa wa Mara umemalizika kwa Igembesabo kuishushia kipigo cha nguvu Mara, magoli 3-0 Mabao yakipatikana dakika ya 73 mfungaji akiwa Kulwa Mobby, dakika ya 78 Fabian James anafunga Bao la pili mara baaada ya mpira wa adhabu toka kwake Jackob Same na kumkuta mfungaji.

Dakika mbili baadae Shinyanga wanaongeza bao la tatu mfungaji akiwa ni yule yule Fabian James, hadi mwisho Shinyanga walitoka kifua mbele kwabao 3-0

Kikosi cha Shinyanga (Igembesabo)

Timu ya mkoa wa Mara.

Timu ya mkoa wa Kagera.
Kesho kutwa katika kituo hiki mchezo wa kwanza saa nane ni baina ya Kagera v/s Shinyanga na mchezo wa pili ni baina ya Mara v/s Mwanza.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.