Kilio kilitolewa juzi na Mwenyekiti wa jumuiya ya Serikali za Mitaa (ALAT), mkoa wa Mwanza Bw. Benard Polycarp kwenye kikao cha kawaida cha jumuiya hiyo kilichoketi katika ukumbi wa jiji la Mwanza.
Polycarp alisema shughuli nyingi za maendeleo za halmashauri zimeshindwa kutekelezeka ipasavyo kwa vile fedha za ruzuku hazijafika kwenye halmashauri hivyo kusababisha shughuli nyingi kulala kwa vile serikali haina fedha.
Alisema wanajitahidi kuendesha halmashauri zao kwa kutumia fedha za vyanzo vya mapato lakini hazitoshi, hivyo alimuomba mkuu wa mkoa kusaidia kupiga kelele ili mafungu ya ruzukuyalipwe haraka kuziokoa halmashauri kujendesha.
“Mheshimiwa mkuu wa mkoa tunaomba utufikishie kilio chetu kwenye ngazi za juu husika tungependa nasi tulipwe mishahara kwa mwezi angalau sh.350,000 na zitambulike kama mshahara” alisema Polycarp.
Bw. Polycarp ambaye ni mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi na diwani wa kata ya Igekelo, alisema wananchi wengi kwenye maeneo yao wana kasumba ya kumwona diwani kuwa ni mtu mwenye uwezo mkubwa wa kifedha hivyo anaposhindwa kutekeleza majukumu kwa kukosa uwezeshwaji wanamhesabu kama mtu asiyejuwa majukumu yake, hivyo hafai.
UPO HAPO!...
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.