ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, January 7, 2011

BILIONEA AAHIDI KUITANGAZA NJE HIFADHI YA SERENGETI.

Mmoja wa matajiri wakubwa duniani, Mukesh Ambani, raia wa nchini India, amemaliza ziara yake katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti na kutoa ahadi ya kuitangaza hifadhi hiyo ili iweze kupata watalii wengi zaidi kutoka mataifa mbalimbali.Ambani anayedaiwa kuwa ni tajiri namba nne duniani, aliingia nchini tangu Septemba 30, mwaka jana kupitia katika Uwanja wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA), akiwa na ndege nne binafsi pamoja na ujumbe wa watu 48.

Tajiri huyo juzi alimaliza ziara yake ya kitalii ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Serengeti, ambapo alipata fursa ya kuzungumza na Waziri wa Maliasili na Utalii, Ezekiel Maige na waandishi wa habari yaliyofanyika katika hoteli ya Bilila Lodge Kempinski, iliyoko ndani ya hifadhi hiyo. Ambani aliahidi kwamba ataitangaza hifadhi hiyo ili iweze kupata watalii wengi zaidi kutoka mataifa mbalimbali.

Katika mazungumzo yake, tajiri huyo mwenye kumiliki majengo makubwa ya kifari nchini India yenye huduma zote (mojawapo hili kushoto) alisema amefurahishwa na kuvutiwa na vivutio vilivyomo katika hifadhi hiyo. Aidha, tajiri huyo alisema ataisaidia Serikali ya Tanzania kutafuta wawekezaji wa kuwekeza katika hifadhi hiyo ikiwa ni pamoja na kujenga mahoteli makubwa ambayo yatavutia watalii wengi zaidi.

Alibainisha kuwa atakuwa balozi mzuri wa Tanzania katika kuitangaza hifadhi ya Serengeti ambayo ina hadhi ya urithi wa dunia, kwani inavyo vivutio vingi wakiwemo wanyama na ndege mbalimbali.

Kwa upande wake, Waziri Maige alisema alifurahishwa mno na ujio wa tajiri huyo na kwamba hiyo ni changamoto kwa Serikali ya Tanzania kwa kuimarisha miundombinu na kuongeza mahoteli katika hifadhi hiyo.




Aliongeza kuwa atashawishi nchi za mashariki ya mbali, kwa kuona uwezekano wa kuwepo usafiri wa uhakika wa ndege, ambao utaunganisha nchi hizo na hapa nchini, hususani katika Jiji la Dar es Salaam ili watalii wengi wapate fursa ya kuja hapa nchini na kutembelea hifadhi mbalimbali.

Tupe maoni yako

1 comments:

  1. gsengo asante sana kwa kuniadd,kila la kheri na kazi njema

    ReplyDelete

Note: Only a member of this blog may post a comment.