ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, January 4, 2011

HALMASHAURI YA JIJI LA MWANZA YAUNDA KIKOSI KAZI KUDHIBITI WEZI WA MIUNDOMBINU YA TAA ZA BARABARANI.

Kutokana na kuwepo hujuma na wizi wa miundombinu ya taa za barabarani halmashauri ya jiji la mwanza kwa kushirikiana na Kikosi cha Polisi imechukuwa hatua ya kuunda kikosi kazi kwania ya kukamata wahalifu ili hatua za kisheria zipate kuchukuliwa dhidi yao.WILSON KABWE.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake mwishoni mwa wiki, Mkurugenzi wa jiji la Mwanza bw. Wilson Kabwe amesema kuwa kufuatia wizi mkubwa uliofanyika kwa nyaya hizo umepelekea maeneo mengi ya barabara kuwa na giza nene hali iliyosababisha kuripotiwa kwa matukio mengi ya wananchi kuvamiwa na wezi, kuumizwa na hata kuporwa malizao.
Bw. Kabwe amewaomba wananchi wa jiji la Mwanza kutoa ushirikiano mkubwa katika kulinda miundo mbinu ya taa hizo sanjari na kufanikisha zoezi zima kwa kutoa taarifa kwa jeshi la polisi ili hatua za kisheria zipate kuchukuliwa dhidi ya wahalifu hao.

BARABARA YA MAKONGORO.

Hivi karibuni usiku wa tarehe 26 Disemba 2010 wezi walichimba na kuondoa nyaya kwenye eneo lote la barabara ya makongoro kuanzia daraja la mirongo hadi maeneo ya Nyakahoja jijini Mwanza hali iliyosababisha mlipukon wa ripoti kubwa ya matukio ya uhalifu.

Ikiwa ni sehemu ya utoaji wa huduma kwa wakazi wa jiji la Mwanza, Halmashauri ya jiji kwa kushirikiana na wawekezaji waliopitishwa kisheria, ilianza kutekeleza mpango wa kuweka taa hizo za barabarani mnamo mwaka 2007. Mpango uliotekelezwa kwa mafanikio makubwa na kuwawezesha wananchi wa jiji la Mwanza kunufaika na uwepo wa taa hizo hasa katika sekta ya usalama wao na mali zao hususani nyakati za usiku.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.